IDARA YA MAJI.
Idara ya Maji ni moja kati ya Idara zilizoko Katika Halmashauri ya Sengerema zenye majukumu yafuatayo:-
Malengo/Majukumu ya Idara ya Maji
Kuandaa bajeti ya kutekeleza miradi ya maji na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo
Kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Halmashauri wasiopata huduma ya maji kutoka kwa mamlaka ya Maji Sengerema.
Kutoa mafunzo, kusimamia mchakato wa kuunda vyombo vya kusimamia na kuendesha miradi ya maji pamoja na kuvisajili, kwa mujibu na taratibu wa Sheria ya Maji ya 2009.
Kuendesha miradi ya maji kutunza fedha za matengezo na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za mfuko.
Kupunguza na kuzuia milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama
Kusimamia vyema miradi inayofanya kazi kwa kusisitiza vyombo vya kusimamia
Idara inahusika na kupanga na kusanifu miradi ya maji, kupitia usanifu wa miradi ya maji unaofanywa na wataalam wa nje, kusimamia ujenzi na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kukarabati miradi ya maji yenye hitilafu. Idara pia inahusika na kuunda na kusimamia vyombo vya watumiaji maji
BODI ZA WATUMIA MAJI.
Idara ya maji imeendelea kukabiliana na changamoto ya miradi mingi ya maji iliyoko vijijini kutofanya kazi vizuri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo kutosimamiwa vizuri na kukosa matengenezo muhimu. Kutokana na dhana kuwa jukumu la kuwapatia wananchi huduma ya maji ni la Serikali pekee, Upungufu huo umesababisha kuhitajika kwa mpango thabiti na endelevu wa uratibu na usimamizi wa utoaji wa huduma hii katika ngazi ya halmashauri ya kuunda Bodi za watumia maji na kuzipa mafunzo pamoja na kusajili Bodi hizo.
MSAJILI WA BODI ZA WATUMIA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA
kupitia Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.12 ya mwaka 2009. Halmashauri za Wilaya, ina mamlaka ya kuteua msajili na kusimamia mchakato mzima wa usajili chini ya Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira, iliyoanza kutumika rasmi tarehe 1.8.2009.
Katika Halmashauri ya Bagamoyo Msajili wa bodi hizi ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Bagamoyo.
UUNDAJI NA USAJILI WA VYOMBO VYA WATUMIAJI MAJI
(i) Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Kijiji au Kamati ya Maji kwa kushirikiana na Wataalam Washauri au Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Wilaya itaitisha kikao cha awali ili kuweka bayana na kujadili wazo la kuunda chombo cha watumiaji maji kwa miradi iliyokwishakamilika, inayoendelea kujengwa au itakayojengwa.
(ii) Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Kijiji itaafikiana kuhusu kuunda chombo cha watumiaji maji na uamuzi huo utawasilishwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji.
(iii) Washauri au Timu ya Wataalam wa Maji na Usafi wa Mazingira ya Wilaya wataelimisha wananchi katika vikao mbalimbali vitakavyoandaliwa, kuhusu umuhimu wa kuunda vyombo vya watumiaji maji vilivyosajiliwa kisheria, aina mbalimbali za vyombo vya watumiaji maji, kuwaongoza na kutoa ushauri katika mchakato wa kuchagua aina ya chombo wanachokipenda, taratibu na hatua za usajili kwa kila aina ya chombo. Chombo cha watumiaji maji kitaanzishwa baada ya wananchi kukubaliana kwa pamoja kwa kuzingatia masharti au vigezo vinavyotawala katika aina ya chombo kitakachochaguliwa.
(iv) Mkutano wa wanakijiji wote utaitishwa ili kuamua kwa pamoja, kwa mujibu wa walio wengi, kuunda aina ya chombo cha watumiaji maji wanachoona kinawafaa kwa mujibu wa maelekezo ya wataalam wa wilaya. Mkutano huo utateua kamati ya muda itakayokuwa na viongozi waanzilishi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia watakaosimamia uundaji wa chombo cha watumiaji maji.
Endapo chombo cha watumiaji maji kitahusisha zaidi ya kijiji kimoja, maamuzi ya wananchi katika kila kijiji yatajadiliwa katika kamati ya muungano yenye wawakilishi wa wananchi kutoka kila kijiji.
(v) Viongozi waanzilishi watasimamia shughuli ya kuandaa rasimu ya katiba na kanuni za chombo kilichopendekezwa.(rejea katiba ya mfano ambayo imeambatanishwa kwenye mwongozo huu). Kwa mujibu wa mwongozo huu, uandaaji wa rasimu ya katiba na kanuni utamshirikisha Mhandisi wa Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mwanasheria wa Halmashauri husika.
(vi) Viongozi waanzilishi walioteuliwa watawasilisha rasimu ya katiba na kanuni kwenye mkutano mkuu wa wanakijiji wote ili kujadiliwa na kupitishwa na mkutano huo.
Iwapo chombo kinachotarajiwa kuundwa kitahusisha kijiji zaidi ya kimoja, rasimu na katiba ya chombo itawasilishwa katika mkutano wa pamoja utakaowajumuisha wawakilishi wa wananchi kutoka vijiji husika, ambao kwa pamoja watafikia maamuzi.
(vii) Pia, viongozi waanzilishi watawasilisha nakala ya rasimu ya katiba na kanuni kwenye kikao cha maendeleo ya kata kwa taarifa, kumbukumbu na pia ili kuthibitisha kutokuwepo kwa pingamizi ndani ya kata. Hii itawezesha kubaini kuwepo au kutokuwepo kwa jumuiya kama ile inayopendekezwa ndani ya kata.
(viii) Baada ya kupitishwa kwa rasimu za katiba na kanuni, mwenyekiti na katibu wa kamati ya muda watawasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri rasimu ya katiba, kanuni na nyaraka zote zinazotakiwa kwa ajili ya uundaji wa chombo cha watumiaji maji, ili kipate ridhaa ya Halmashauri. Mkurugenzi wa Halmashauri ana uhuru wa kufanya ukaguzi au uchunguzi wowote anaouhitaji kupitia wataalam wake ili kujua hali halisi, kabla ya kuwasilisha ombi la kuunda chombo kwenye kamati au vikao husika kwa ajili ya kupata ridhaa.
(x) Mkurugenzi wa Halmashauri atakiandikia barua chombo husika kilichoundwa, akionyesha kuwa Halmashauri imetoa ridhaa ya kuundwa kwa chombo husika katika kijiji/vijiji kilichowasilisha maombi hayo, akiambatanisha majina ya viongozi waanzilishi (Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina) wa chombo husika kwa kuzingatia matakwa ya katiba na atatoa nakala kwa Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kijiji.
(xi) Kufikia hatua hii, chombo cha watumiaji maji tayari kitakuwa kimeundwa kulingana na katiba na kanuni walizojiwekea, tayari kwa hatua za usajili.
USAJILI WA VYOMBO VYA WATUMIAJI MAJI
(i) Viongozi wa chombo cha watumiaji maji watawasilisha fomu ya maombi ya kusajili chombo cha watumiaji maji kwa Msajili na kutoa nakala kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Afisa Mtendaji wa Kata, wakiambatanisha katiba na kanuni ya chombo hicho na muhtasari wa mkutano mkuu wa wanakijiji/wanavijiji wote pamoja na majina ya wajumbe waliohudhuria na sahihi zao na nakala ya barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri inayoonyesha kuwa Halmashauri imeridhia uundaji wa chombo hicho.
(ii) Waombaji watalipia ada ya usajili wa chombo cha watumiaji maji kama itakavyopangwa na Msajili wa Vyombo vya Watumiaji Maji wa Halmashauri.
(iii) Msajili atahakiki uhalali wa chombo cha watumiaji maji kilichofuzu vigezo vilivyotakiwa kwenye usajili na kutoa mapendekezo au ushauri kwa chombo ambacho hakikufuzu ili kizingatie vigezo na kiweze kufuzu.
(iv) Wananchi watafahamishwa kuhusu matokeo ya uhakiki iwapo maombi yao yanafuzu vigezo vilivyowekwa au kama yanahitaji maboresho kabla ya kusajiliwa.
(v) Msajili atatoa hati ya kisheria ya usajili kwa chombo cha watumiaji maji kilichofuzu vigezo vilivyotakiwa ili kitambulike kisheria na kuweza kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa mujibu wa sheria.
(viii) Msajili atatoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu maombi yaliyopokelewa, kuhakikiwa, kukubaliwa na kusajiliwa ama kukataliwa.
(ix) Waombaji ambao maombi yao yamekataliwa wanayo haki ya kukata rufaa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri baada ya kulipa ada kama itakavyopangwa na msajili.
Baadhi ya Maeneo yaliyopo ndani ya Halamsahauri ambayo yana miradi ya maji inayoendelea
Mradi wa maji buyagu, kalangalala, Bitoto
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.