Kutafsiri Sera za maendeleo kulingana na Halmashauri ya Sengerema na kufanya mrejesho kwa wadau wa maendeleo.
Kuunganisha na kuhakikihatua za upangaji wa mipango ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia sera za kitaifa.
Kutekeleza sera ya mipango na idara ya watu kwa kukusanya takwimu mhimu na kufanya mrejesho kwa wadau wa maendeleo.
Kuwezesha maendeleo ya haraka kwa jamii kwa kuwashirikisha wadau katika hatua za upangaji wa mipango ya maendeleo na katika kutoa mrejesho wa taarifa za maendeleo.
Kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya uanzishwaji wa shughuli za maendeleo.
Kuandaa mipango na bajeti ya mwaka kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali na uendeshaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema.