MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina jukumu la kutoa angalizo na ushauri kwa taasisi kuhusiana na jinsi taasisi inavyotekeleza majukumu yake ya msingi. Huduma za ushauri ambazo Kitengo huzitoa ni zile zenye lengo la kuongeza ufanisi wa Taasisi.
Kwa upande wa Halmashauri za Serikali za Mitaa, wakaguzi wa ndani wanatoa maangalizo na ushauri wenye lengo la kuboresha huduma zitolewazo kwa wananchi. Ushauri na maangalizo haya yanapaswa kutolewa kwa uhuru na yanalenga kuiwezesha Halmashauri kufikia malengo ambayo imejiwekea. Majukumu ya Wakaguzi wa ndani yanapaswa kutekelezwa kwa utaratibu uliopangwa vizuri na wenye kuzingatia miiko ya taaluma na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
Pia kuona kama mifumo mbalimbali ya udhibiti iliyowekwa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa. Kitengo cha Ukaguzi wa ndani kinafanya kazi zake kwa kuchambua mifumo ya udhibiti na kufanya tathmini ya kiwango cha uzingatiwaji wa mifumo hiyo katika utekelezaji wa majukumu ya siku kwa siku na kisha kutoa ushauri na maangalizo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.