Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji (w) kuhusu masuala yote yanayohusu Utawala na Utumishi katika Halmashauri.
Kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu nidhamu ya Watumishi katika Halmashauri.
Kusimamia na kuratibu upimaji wa utendaji wa kazi kwa watumishi kwa kuzingatia Sera ya Menejimenti na Ajira katika utumishi wa Umma.
Kusimamia, kutafsiri kwa kuzingatia Sera, Kanuni na Taratibu za mafunzo ya kiutumishi kama yalivyoidhinishwa na Serikali na kushiriki katika kutoa mafunzo.
Kuratibu na kusimamia taratibu za kuajiri na kupokea watumishi wapya katika Halmashauri.(Mkuu wa Idara ndiye Katibu wa Bodi ya Ajira katika Halmashauri).
Kuratibu na kusimamia taratibu za kuthibitishwa kazini na upandishwaji vyeo kwa watumishi wa Halmashuri isipokuwa Walimu.
Kutathimini mipango ya mafunzo ili kupima mafanikio au kutofanikiwa na kushauri marekebisho yanayohitajika.
Kuainisha na kushauri kuhusu mpango bora wa mahitaji ya watumishi.
Kutunza na kuboresha takwimu za mahitaji ya watumishi katika Halmashauri
Kusimamia na kuratibu matumizi au mpangilio bora wa nyumba na ofisi za
Halmashuri. (Mkuu wa Idara ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Nyumba.
Kusimamia na kuratibu matumizi ya magari na usafiri katika Halmahuri.
Kupokea, kuratibu na kushughulikia malalamiko ya watumishi kutokuwa na Dawati la Malalamiko)
Mkuu wa Idara ndiye Katibu wa Kamati ya Maadili ya Madiwani
Kuratibu na kusimamia maandalizi ya makisio ya mishahara ya Watumishi (PE) katika Halmashauri.
Kuratibu uandaaji wa orodha ya ukubwa kazini (Tange) kila mwaka nakuiwasilisha OR- TAMISEMI kwa wakati.
Kusimamia masuala ya usafi wa mazingira ndani na nje ya ofisi za Halmashauri.
Kusimamia utendaji kazi wa watendaji wa Kata na Vijiji.
Kuandaa taarifa za Idara za Robo, Nusu na Mwaka.
Kuratibu Vikao vya Menejimenti, Kamati mbalimbali na Mikutano ya Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na Makatibu wa Kamati
Kuratibu masuala ya mirathi.
Kuandaa mpango wa mafunzo kwa kushilikiana na Wakuu wa Idara/ Vitengo.
Kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu Utawala Bora.