SERIKALI KUVUNA 20% MKATABA WA NYONGEZA NA NYANZAGA
Leo tarehe 20 Agosti, 2025 serikali na kampuni ya nyanzaga mining company limited wamesaini makubaliano ya nyongeza kwaajili ya uchimbaji wa Madini aina ya dhahabu kupitia kampuni ya ubia ya sotta mining corporation limited.
Akizungumza na wananchi kwenye hafla ya utiaji saini katika kijiji cha sotta-Igalula wilayani sengerema Waziri wa Madini mhe. Antony Mavunde Amesema nyongeza hiyo ya makubaliano ya hisa zilizofifishwa utaongeza hisa 4% kwa serikali kutoka 16% hadi 20% huku hisa za mwekezaji zikishuka kutoka 84% hadi 80% kutoka katika mkataba wa awali.
Naye mkuu wa Mkoa wa mwanza mhe. Said Mtanda amesema kupitia mgodi Huo maisha ya wananchi wa sengerema na mwanza kwa ujumla yatainuka kiuchumi na kusaidia Pato la taifa kwa wastani wa kutoka 7.5% ya sasa hadi 10% ikiwa Ndio malengo ya mkoa umejipangia.
|
|
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.