Muundo wa Idara:
Idara ya Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili ambazo ni:
Majukumu ya Idara:
Jukumu kuu la Idara ni pamoja na usimamizi wa shughuli zote zinazohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Sengerema kwa kushirikiana na Serikali Kuu na Wadau mbalimbali katika sekta. Baadhi ya shughuli hizo ni pamoja na:-
1 Kusimamia shughuli za udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ya mifugo ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo.
2. Kusimamia ubora na usalama wa mazao yatokanayo na mifugo na uvuvi
3. Kuratibu na kusimamia sheria mbali mbali za mifugo na uvuvi
4. Kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazohusiana na maandalizi na ushiriki wa mikutano ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na sherehe mbalimbali za mifugo na uvuvi
5. Kusimamia na kuratibu shughuli zinazofanyika katika umiliki wa Halmashauri kama majengo ya Halmashauri yaliyopo chini ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kama vile; machinjio
6. Kusimamia mapato yatokanayo na ushuru wa Mifugo, samaki na mazao yake.
7. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiutawala na utumishi wa wataalam wa mifugo na uvuvi.
8. Kuratibu na Kusimamia ukusanyaji wa ushuru, tozo, ada, na leseni zinazohusiana na sekta ya mifugo na uvuvi.
A: KITENGO CHA MIFUGO
Halmashauri ina mifugo mbalimbali kama ifuatavyo:- ng’ombe, mbuzi, Kondoo, Nguruwe, Kuku na Punda.
1.Majukumu ya kitengo cha Mifugo
2.Kusimamia sera, sheria na kanuni za mifugo
3. Kusimamia na kudhibiti utoaji wa huduma za ugani
4. Kukusanya na kutunza takwimu mbalimbali za Mifugo(idadi ya mifugo, uzalishaji, magonjwa ya mifugo na huduma nyinginezo)
5. Kuratibu na kusiamaia ubora na usalama wa mazao ya Mifugo kwa usalama wa jamii
6. Kutoa ushauri juu ya njia sahihi za kuzuia magonjwa ya Mifugo (tiba, kinga/chanjo na uogeshaji)
7. Kusimamia utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ya mifugo (Majosho, Minada, Malambo na Machinjio)
8. Kuratibu na kusimamia shughuli za usafirishaji wa mifugo na mazao yake
9. Kusimamia usambazaji wa pembejeo za mifugo na kuwezesha sekta binafsi kutoa huduma za mifugo
10. Kufanya ukaguzi wa nyama na kutoa elimu ya uchunaji bora wa ngozi
11. Kushirikiana na taasisi mbalimbali za utafiti katika sekta ya Mifugo
12. Kutoa elimu juu ya uzalishaji, utunzaki na uendelezaji wa nyanda za malisho.
MAENEO YA UWEKEZAJI
1.Uchakataji wa mazao ya mifugo kama vile Maziwa, ngozi na nyama
2.Ujenzi wa machinjio ya kisasa
3.Ujenzi wa miundombinu ya masoko ya mifugo( mnada)
4.Uzalishaji wa mbuzi na mitamba ya kisasa kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa
MAGONJWA YA MIFUGO
Baadhi Magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (Zoonotic diseases)
1. Kimeta
2. Kifua kikuu
3. Typhoid
4. Colibacillosis
5. Kichaa cha mbwa
6. Leptospirosis
7. Brucellosis
BAADHI YA MAGONJWA YA NG'OMBE
1.Ndigana kali
2.Ndigana baridi
3.Chambavu
4.Kimeta
5.Ndorobo
6.Homa ya mapafu.
7.Midomo na miguu
8.Ugonjwa wa kiwele
9.Maji moyo
10.Minyoo
11.Ugonjwa wa ngozi( Lumpy Skin)
12.Ugonjwa wa kutupa mimba(brucellosis)
Baadhi ya magonjwa ya mbuzi na Kondoo
1. Maji moyo
2. Homa ya mapafu
3. Sotoka ya Mbuzi na kondoo
4. Minyoo
Baadhi ya Magonjwa ya jamii ya ndege
1. Mdondo (Newcastle disease)
2.Koksidiosisi
3. Koryza (mafua)
4. Ndui
5. Minyoo
6. Typhoid
7. Colibacillosis
Magonjwa sumbufu na hatari kwa mbwa
1. Kichaa cha Mbwa
2. Leptospirosis
3. Kuhara damu (canine parvovirus infection)
4. Canine Distemper
5. Canine hepatitis
Magonjwa yanayozuilika kwa kutoa chanjo ni:-
Kimeta na chambavu kwa ng`ombe, mbuzi na kondoo
1. Ndigana kali - ng`ombe
2. Homa ya mapafu kwa Ng`ombe na Mbuzi
3. Lumpy skin- Ng`ombe
4. PPR – mbuzi
5. Kutupa mimba (Brucellosis)-Ng`ombe
6. FMD- Ng`ombe
7. Kichaa cha mbwa – mbwa na paka
8. Distemper, Hepatitis, Leptospirosis na Parvovirus(DHLP)-Mbwa
9. Newcastle disease – jamii ya ndege
10. Gumboro
11. Ndui
12. Typhoid
13. Mareck`s disease
Namna ya kupata na kutumia chanjo
Chanjo zinapatikana kwenye maduka/vituo vya kuuzia pembejeo za Mifugo. Pia unaweza kuwasiliana na Wataalam wa mMifugo kwa elimu na msaada zaidi.
KITENGO CHA UVUVI
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UVUVI.
1. Kutekeleza Sera ya Uvuvi.
2 .Kusimamia uhifadhi wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao.
3 .Kuratibu na kusimamia uhifadhiwa samaki na viumbe wengine wa baharini.
4. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora wa samaki na mazao ya uvuvi,Biashara na Masoko ya samaki pamoja na Ufugaji samaki na viumbe wengine wa majini.
5. Kutoa leseni za uvuvi
6. Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi.
7 .Kusimamia na kutekeleza Sheria za Uvuvi.
8. Kusimamia ukusanyaji wa Takwimu na maduhuli.
9. Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi.
10.Kutoa ushauri juu ya uendelezaji wa matumizi ya rasilimali za uvuvi.
11.Kukagua ubora wa samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya Kitaifa
MAENEO YA UWEKEZAJI YALIYOPO NA YANAYOHITAJI UWEKEZAJI
1.Ufugaji wa samaki katika mabwawa (uliopo).
2.Kiwanda cha uchakataji samaki (unaohitajika)
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.