Halmashauri ya wilaya ya Sengerema imeazimisha siku ya kumbukizi ya mauaji ya watu wenye Ualbino, walio-uwawa na kujeruhiwa kutoka 2004-2025, ambapo Sengerema liliripotiwa tukio la kwanza la mauaji mwaka 2006 katika kijiji cha kashindaga kata ya Igulumuki.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya sengerema kwa kushirikiana na Taasisi ya UNDER THE SAME SUN kwa kuthamini na kuonyesha upendo kwa watu wenye ualbino.
Kwa upande mwingine Mkuu wa wilaya ya Sengerema amehimiza jamii kuimarisha ulinzi , usawa na kuzuia ukatili kwa watu wenye ualbino, pia ametoa rai kwa waganga wa jadi kuepukana na ramli chonganishi zinazopelekea kuua watu wenye ualbino na kuchukua viungo vyao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Ndug. Binuru Shekidele amewasihi wananchi wa sengerema waishi kwa usawa pasipo kubaguana kwani binadamu wote ni sawa,
Nae Muhasisi wa shirika la Under the same sun ndug Peter Ashy amehimiza usawa kwa binadamu wote “Disability is not inability” na pia kuwawezesha na kuwapa nafasi mbalimbali za madaraka kwa watu wenye ualbino kwani wanaweza kuleta matokeo chanya kwa jamii kama ilivo kwa wengine.
Maadhimisho ya kumbukizi ya mauaji ya watu wenye ualbino yanafanyika mwezi july kila mwaka, kwa Halmashauri ya wilaya ya sengerema yamefanyika tarehe 29 july 2025 katika viwanja vya redio sengerema .
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.