HALMASHAURI YA SENGEREMA YAADHIMISHA KILELE CHA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA Halmashauri ya Sengerema leo tarehe 20-8-2025 imeadhimisha kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikisisitiza umuhimu wa elimu endelevu kwa maendeleo ya jamii. Akifungua maadhimisho hayo,Bi.Genoveva Chuchuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri alisema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu ya watu wazima ili kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kujifunza bila kujali umri, kwa lengo la kuongeza ujuzi, kupunguza ujinga na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, aliwataka wananchi kushirikiana kikamilifu katika programu za elimu ya watu wazima ili kufanikisha azma ya taifa ya kujenga jamii yenye maarifa na stadi za maisha kwa maendeleo endelevu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.