Halmashauri ya Sengerema ina eneo la hekta 164,184 zinazofaa kwa kilimo cha mazao ya chakula na Biashara. Eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 95,789. Katika msimu huu, Halmashauri imelenga kulima jumla ya hekta 88,820 kati ya hizo hekta 72,595 ni mazao ya chakula na hekta 16,255 mazao ya biashara. Mazao ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mahindi, Mtama, Mawele, Mihogo, Mpunga, Viazi vitamu, Maharage, Kunde, Njugumawe, karanga na Choroko. Mazao ya biashara ni Pamba, Dengu na Alizeti. Halmashauri yetu inapata mvua katika misimu miwili vuli na masika, ambapo mwaka huu mvua zimepatikana za kutosha. Hali ya upatikanaji wa chakula ni ya wastani, kwa sasa Halmashauri inajitosheleza kwa chakula ingawa bei zinaendelea kupanda kutokana na uzalishaji kuwa chini.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.