Halmashauri ina vituo vya kutolea huduma za afya 53 vinavyomilikiwa na Serikali vipo 48, mashirika ya kidini 01 na watu binafsi 04. Pamoja na huduma nyingine vituo hivi hutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD), mama na mtoto, ushauri nasaha (CTC) na kutoa huduma za afya mashuleni. Kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Mei 2023 Halmashauri imefanikiwa kupokea jumla ya Tshs. 4,108,811,867.30/= kwa mchanganuoufuatao:- Tshs. 750,000,000/= kwa ajili ya kujenga majengo manne katika Hospitali ya Wilaya. Vifaa tiba vyenye thamani ya Tshs. 418,000,000/= vimepokelewa kwa ajili ya jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya (Serikali kuu), Tshs. 200,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa kituo cha Afya kimoja na Zahanati tatu (Serikali kuu), Tshs. 50,000,000/= kwa ajili ya ukamilishaji wa boma 01 ya Zahanati ya Lugongo (Serikali kuu) Tshs. 2,690,811,867.30 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji nausafi wa mazingira katika vituo 39 (SRWASS).