Mratibuwa SLEM wa Halimashauri ya Sengerema Bwn. Kasasiro Boniphace amesema mradi huuwa slemu ulianza mwaka 2009 na mpaka sasa ni vikundi 574 vimenufaika na mpangohuo na hii ni awamu ya 25 tangu mpango wa kupatia fedha vikundi hivi uanze.
Lengo ni kuinua kipato cha wananchiwa kipato cha chini wilayani ili waweze kujikwamua na umasikini ambaposerikali iliona njia pekee ya kuwakomboa wananchi wake ni kuundavikundi na kufanya kazi kwa pamoja ikiwa ni masharti ya kuweza kupatiwa mkopo nakuhakikisha walioomba na kupata mkopo huu wanautumia kwa matakwa waliyokusudiwaili kufikia malengo.
Huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaSengerema Bwn. Magesa Boniphace akisema mkopo huu utatudumu kwa miezi 6 ambapowanatakiwa kurejesha ili na vikundi vingine vipate furusa ya kupata haki yakukopa mikopo hii .
Akizungumuza katika hafla ya uzinduzi wa utoajiwa hundi za mikopo hiyo kwa vikundi vya wajasiliamali Mkuu wa Wilaya yaSengerema Bwn. Emmanuel Kipole amesema kuwa serikali imedhamilia kuibadilishanchi kwa kufanya kazi na mtaji ni wananchi wenyewe,hivyo waliopata mkopo huuwanatakiwa kuutumia vema na kurejesha kwa wakati ili kutoa furusa kwa wenginenao waweze kukopa.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.