Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Nchengerwa amefanya ziara katika wilaya ya Sengerema na kupata fursa ya kuzungumza na wanufaika wa Mpango wa kaya maskini lengo ikiwa ni kujionea hali halisi jinsi ambavyo zoezi la kuandikisha kaya mpya limefanyika.
Akizungumza na walengwa wa mpango wa kaya maskini (TASAF) katika kijiji cha Katunguru amewaagiza watendaji wa TASAF ngazi ya wilaya kuhakikisha wanajiridhisha na kaya zote ambazo hazikuingizwa katika mpango zinaingizwa ili kila mwananchi mwenye sifa aweze kunufaika mradi wa mpango wa kaya maskini.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.