Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Said Jaffo ametoa onyo hilo alipofanya ziara katika Halmashauri ya Sengerema, alipokuwa akizungumza na wananchi katika ukumbi wa halmashauri.
Mhe.waziri ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi wa Maji Buyagu, na kumwagiza mhandisi wa maji wilaya ya sengerema Ndg. Nicas Ligombi ifikapo 30 Feburuari 2018 mradi huo uwe umekwisha na yeye mwenyewe atarudi kuja kufanya ufatiliaji huku akisema ikitokea mradi huo hautoi maji basi Mhandisi atafute mahali pa kwenda. amesema “haiwezekani mradi toka 2014 mpaka leo maji hakuna”
Huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na miongozo ya majukumu yao, pia kuachanan na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza ufanisi na tija katika kuwaletea maendeleo wananchi na taifa kwa ujumla.
Pia amewaagiza watumishi wote nchini kuwa na mipango mikakati na malengo ya kujipima katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanizi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na amewaomba wakuu wa idara kubadirika na kuacha kujifanya miungu mtu katika idara zao, ikiwa ni pamoja kuzingatia usawa kwa watumishi wote waliochini yao.
Huku akisisitiza upendo na amani mahala pa kazi ni jambo la mhimu hivyo viongozi wote muwe mfano katika kufanya sehemu zetu za kazi zinakuwa mahala salama ili watumishi wetu wafanye kazi wakiwa na utulivu wa akili na amani mioyoni mwao, kwa anaamini bili utulivu wa aikili nafsini ni ngumu kuwa na ufanisi katika majukumu ya kila siku.
Nae katibu Tawala wilaya ya sengerema Ndg. Agustin Allan, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amemshukuru Mhe. Waziri na kumwahidi kuwa watazingatia yale yote aliyowaasa na kuyafanyia.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.