• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI NDUMBARO AWEKA JIWE LA MSINGI UWANJA WA MICHEZO SENGEREMA

Posted on: July 3rd, 2024


Uwanja sasa kuitwa TABASAMU

Sengerema Sekondari Kunufaika Miundombinu ya Michezo

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, leo Julai 3, 2024 ameweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa Uwanja wa Mnadani uliopo mjini Sengerema ambapo kupitia hotuba yake ameupa jina  Uwanja huo na kuwa uwanja wa Tabasamu kutokana na mchango mkubwa wa kufanikisha ujenzi huo uliotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. Hamis Tabasamu kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.


Akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi iliyofanyika uwanjani hapo Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema kupitia juhudi za Mbunge, Halmashauri na wadau wengine ni vyema uwanja huo ukapewa jina la Tabasamu kwani amekuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa uwanja huo na ametumia fedha za mfuko wa jimbo pamoja na mchango wake binafsi kufanikisha ujenzi wa uwanja huo ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuandaa andiko la maombi ya fedha litakalowasilishwa Wizarani ili kuweza kusaidia kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.


"Na mimi leo naubadilisha jina huu uwanja huu wa Mnadani na kuitwa uwanja wa Tabasamu, Mhe. Mbunge kwa kushirikiana na Halmashauri na ninyi wananchi mmefanya jitihada kubwa kufanikisha ujenzi wa uwanja huu" amesema Dkt. Ndumbaro.


Awali Waziri Dkt. Ndumbaro alitembelea Sekondari ya Sengerema ambapo Serikali imepanga kujenga miundombinu mbalimbali ya michezo ikiwa ni miongoni mwa shule 56 za michezo zitakazojengwa nchini.


Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe. Hamis Tabasamu amesema ujenzi wa uwanja huo kwa awamu ya kwanza ulianza tarehe 1 Aprili, 2024 na unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 360 ambapo ujenzi umefikia asilimia 75.


Amesema awamu ya pili ya ujenzi uwanja huo itakuwa ni ujenzi wa eneo la kuchezea na pamoja na uwekaji wa majukwaa ya watazamaji pamoja na taa za uwanjani kwa awamu ya tatu hivyo amemshukuru mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na amemwomba Waziri Dkt. Ndumbaro kupitia Wizara ya Michezo kusaidia ukamilishaji wa uwanja huo ambao unazo sifa zote za kuwa uwanja wa kisasa na ambao unaweza kutumika katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema, Mark Agustine Makoye amesema ujenzi wa uwanja wa michezo katika mji wa Sengerema ni hitaji la muda mrefu kwa wananchi hivyo amewaomba wananchi wa Sengerema kuwa tayari kuutumia uwanja huo ambapo vipaji  vingi vya wanamichezo vitaibuliwa.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.