Ataka Halmashauri kuanzisha miradi ya kimkakati
Aweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Halmashauri, Jengo la Utawala
Daraja la JP Magufuli kuzinduliwa na Dkt. Samia Juni 19, 2025
*Umoja wa Bodaboda Sengerema Wachangiwa Milioni 50 Kununua Gari la Abiria
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesifu jitihada za Serikali wilayani Sengerema kwa kusimamia vyema fedha za miradi ya maendeleo ambapo amesema Wilaya ya Sengerema imepiga hatua kubwa kimaendeleo ndani ya muda mfupi ambapo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuanzisha miradi ya kimkakati ili kuvutia wadau mbalimbalimbali wa maendeleo wakiwemo watalii.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Mei 19, 2025 wakati wa ziara yake wilayani Sengerema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya stendi ya zamani mjini Sengerema.
Waziri Mkuu amesema kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo Sengerema pamoja kukamilika kwa daraja la Kigongo Busisi kukamilika na Mgodi mkubwa uliopo Nyanzaga, viongozi wa Halmashauri wanatakiwa kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kimkakati likiwemo soko la kisasa, stendi pamoja na maegesho ya magari ili kuvutia wafanyabiashara mbalimbali pamoja na watalii kuja wilayani Sengerema kuwekeza.
"Niwapongeze kwa ujenzi wa Soko na stendi, Sengerema inakua kwa kasi, ninyi hamuwezi kuona, Sengerema imakuwa kwa kasi, Sengerema ni mji wa kibiashara, Sengerema kuna idadi kubwa ya watu, na kuna mgodi mkubwa utaanza hivi karibuni, hapa patakuwa hapashikiki" amesema Waziri Mkuu
Wakati huo huo Waziri Mkuu amepongeza jitihada za umoja wa Bodaboda Wilayani Sengerema kwa kuamua kununua gari la abiria ambapo yeye mwenye, viongozi na umoja wa Bodaboda wamechangia kiasi cha shilingi milioni 50 kuwezesha upatikanaji wa gari hilo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amesema ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi lenye urefu wa kilometa 3 kwa sasa umekamilika, ambapo amesema sasa litazinduliwa rasmi tarehe 19 Juni, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Mbunge wa jimbo la Sengerema Mhe. Hamis Tabasam amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo katika jimbo la Sengerema ambapo amemwomba Waziri Mkuu kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa hospitali ya Wilaya iliyopo Mwabaluhi kwa kujenga uzio pamoja na nyumba za watumishi.
Mapema Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya Hamashauri pamoja na jengo la utawala lililopo Bomani.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.