Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole ameahidi kutafuta fedha kwa wahisani mbalimbali kwa lengo la kujenga kituo cha wazee wilayani sengerema ili kuwajengea uwezo wa kukutana na kubadilishana mawazo.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa mgeni Rasimi katika hafura iliyoandaliwa na wazee hao kwa ajili ya kumpongeza Rais John Magufuri kwa kazi anayoifanya ya kuhakisha rasilimali za nchi zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania.
Alisema nijambo la kujivunia kwa wazee hawa kukutana na kumpongeza rais wetu kwa kazi anazozifanya kama wazee wameona na kumpongeza tunapaswa kuungajuhudi hizi kwa kuwasaidia mahitaji yao waliyomba ya kupatiwa eneo la kujenga kituo chao.
‘Mimi kama kuu wa wilaya ya Sengerema tutashirikiana na mkurugenzi kutafuta wahisani popote ili tupate milioni 200 kwa ajiri ya kuwajengea kituo wazee hawa waliounda kikundi chao kwa ajili ya kufanya shunguri zao kwa pamoja na kujipatia maendeleo’ amesema Kipole.
Nae Mwenyekiti wa umoja wa wazee kata ya Nyampulukano amesema kikundi hicho kinawanachama 102 wanawake kwa wanaume kimeanzishwa mwaka 2014 na kinausajili katika ofisi ya maendeleo ya jamii na lengo la kuanzishwa kwa kikundi hiki ni kubuni miradi ya kujipatia kipato kama wazee.
Amesema kama wazaee tulikaa na kujadili kukutana leo;jana ikiwa lengo ni kumpongeza Rais na kutoa kiliochetu kwa Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kutusaidia kupata eneo la kujenga kituo chetu, ombi ambalo limekubali na hivyo watapatiwa eneo kujenga kituo kitu ambacho ni jambo la kushukuru kwa kuwa viongozi wameona ni busara kusaidia wazee hao.
Mmoja wa wazee hao Bwn. Sesilia Mchanga amesema kuwa hatuna budi kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kulinda rasilimali za nchi hivyo tunapaswa kuwaombea viongozi wetu kwa juhudi hizo na sisi kama wazee tuko tayari kutoa ushirikiano wa pamoja katika swala zima la kutoa ushauri juu ya maswala yoyote ya mstakabali nchi yetu.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Sengerema Magesa Mafuru amesema kuwa atafanya mchakato wa kupatikana kwa kiwanja cha kujenga kituo cha wazee wilyani hapa kwa kuwa jambo hilo liko ndani ya uwezo wake.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.