Jumla ya watoto wenye ulemavu 55 wametajwa kushindwa kupata Elimu kutokana na wazazi kutowapeleka shule katika Kata ya Chifufu wilayani Sengerema Mkoani Wwanza.
Hayo yamebainishwa na mwalimu wa kitengo maalumu wa shule ya msingi Chifufu Bi. Magreth Kaboya wakati akisoma taarifa mbele ya Mgeni rasim katika maadhimisho ya piga kengele yaliyofanyika katika kata ya chifufu,na kueleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Akijibu risala hiyo Bwn Pius Lwamini ambaye ni afisa Elimu taaluma shule za msingi Halmashauri ya Sengerema kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya sengerema Mhe. Emmanueli Kipole amewagiza viongozi wa Kata ya Chifufu kuhakikisha wanawachukulia hatua kali za kisheria wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu.
Katika maadhimisho hayo jumla ya fedha taslimu laki moja, thelathin na tano Elfu, pamoja na mifuko 5 ya saruji zimechangwa kwa ajili ya ujenzi shule hiyo.
Maadhimisho hayoyenye kauli mbiu "Waatoto wote wana haki ya kuwa Shuleni, kupata Elimu Bora wakiwemo Watoto wenye Ulemavu"
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.