Katika maadhimisho ya Siku yaMtoto wa Africa yaliyofanyika katika kijiji cha Chifunfu kata ya Chifunfu wilayani Sengerema. Watoto kupitia risala iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mhe. Mkuu wa Wilaya, aliyewakiliswa na Katibu Tawala Bw. Allan Agustine.
Wameiomba serikali kuhakikisha inaziondoa au kuzifanyia marekebisho sheria zote ambazo ni kandamizi na hazina tija kwa ustawi wa maendeleo ya mtoto.
Pia wameiomba jamii kuzingatia haki za watoto katika ngazi ya familia na jamii nzima kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtoto anapata haki ya kupewa elimu, haki ya kupata malezi, haki ya kutokutumikishwa kazi sehemu za viwandani pamoja na haki ya kupumzika.
Akijibu maombi hayo mgeni rasmi katika hutuba yake amewahaikishia kuwa serikali ipo pamoja na watoto wote nchini na kwa kuonyesha kuwa ina dhamira ya dhati imeamua watoto wote wanapata elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.
Serikali inaendelea kufanya marekebisho mbalimbali ya sheria za mtoto lengo ikiwa nikuhakikisha mtoto anapata haki zake za msingi.
Nae Kaimu Mkurugenzi Bw. Malulu akitoa salamu zake kwa watoto kabla ya kuhitimishwa kwa maadhimisho na mwenyekiti wa baraza la watoto kiwilaya ameukumbusha umma kuona umhimu wa matukio haya ya kitaifa ambayo watoto wetu mnamo tarehe 16 mwezi 6 1976 huko South Africa waliuwawa kwa kudai haki zao za msingi hasa haki ya elimu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.