Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema imeadhimisha ya siku ya wanawake duniani huku ikitoa mikopo ya shilingi milioni 362 kwa vikindi 111 vya wa wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mhe. Senyi Ngaga ameipongeza Halmashauri ya Sengerema kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha kwa mara ya kwanza kwa vikundi hivyo ambapo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kurejesha fedha hizo ili ziweze kunufaisha vikundi vingine.
"Miaka yote Halmashauri imekuwa ikitoa mikopo milioni mia, mia na kitu, lakini kwa mara ya kwanza leo zinatolewa milioni 362, tumpongeza Mhe. Dkt. Samia kwa kuamua kuweka utaratibu mzuri wa mikopo hii ambao leo tunaona matunda yake" amesema Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo wilayani Sengerema hususan kwa wananchi wa vijijini ambapo katika Halmashauri ya wilaya ya Sengerema pekee kwa mwaka 2025 inafungua shule mpya 15 za Sekondari ikiwemo shule mpya ya ufundi ya Tabaruka sambamba na kuongezeka ufaulu kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024 ambao umetokana na uwepo wa miundombinu mizuri kwenye shule hizo pamoja na uwepo wa walimu wa kutosha.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wajasiriamali wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Bibi. Darling Matonange ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kwa kutoa mikopo hiyo kwa makundi hayo ambapo imeweza kuwasaidia kujikomboa kiuchumi ambapo ameomba kuongeza kiasi cha fedha ili vikundi vingi viweze kunufaika na mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ally Salim amesema mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi hivyo ambavyo vimekidhi vigezo hivyo ameviomba vikundi vingine vyenye sifa kuendekelea kuomba mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi, kwa Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema yamefanyika tarehe 5 Machi kwenye viwanja vya stendi ya zamani ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; *Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji*
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.