Katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siki ya wanawake duniani tarehe 8 Machi, 2025, umoja wa wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, leo Machi 3, 2025 wametoa misaada na zawadi mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji pamoja na wagonjwa katika hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema (DDH).
Akiongea wakati wa kukabidhi zawadi na misaada hiyo, mwenyekiti wa umoja huo Darling Matonange amewashukuru wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kwa moyo wa kujitolea kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji kwenye kituo cha Busitani C pamoja na wagonjwa katika hospitali teule ya Sengerema.
"Tumekuja hapa kwa sababu sisi ni kina mama ambao tunaguswa sana na malezi ya watoto, wakina mama tunayo nafasi kubwa kwenye malezi huko majumbani, hivyo tunaguswa kufanya matendo ya huruma kwa hawa watoto wetu" amesema Bibi Matonange.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Meriejose amewashukuru wanawake hao ambao wamejitokeza kutoa misaada mbalimbali ambao amesema katika kituo cha Bustani C wanao watoto ambao ni yatima, watoto wanaosubiri matibabu pamoja na wenye changamoto za ukatili majumbani.
Misaada na zawadi iliyotolewa ni pamoja na vyakula kwenye na mafuta ya kupikia, mahitaji ya shule vinywaji, ungalishe na mafuta ya kupaka.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo kiwilaya maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 5 Machi, 2025 na kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni *Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”*
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.