• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DED SENGEREMA AGUSWA NA KERO ZA WATUMISHI

Posted on: May 2nd, 2025

Kero Mbalimbali Zatatuliwa


*Watumushi Wapongeza zoezi hilo*

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wametakiwa kudai haki  zao za kiutumishi wawapo katika utumishi na kuepuka kusubiri wakati wa kustaafu.


Wito huo umetolewa leo Aprili 28, 2025 na Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema Ndugu Curthbert Midala kwenye kikao cha kusikiliza na kutatua kero za watumishi mbalimbali wa tarafa ya Sengerema kilichoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na kufanyika kwenye ukumbi wa Sekondari ya Sengerema.


Kupitia kikao hicho Katibu Tawala Wilaya amewataka watumishi hao kutokuchoka kudai haki zao wawapo katika utumishi kwani kupitia utatuzi wa changamoto hizo kutasababisha utendaji kazi mahili kwa watumishi sambamba na utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi kwenye ngazi za vijiji kwa wakati.


"Mambo yetu sisi watumishi tuyafuatilie wakati tupo katika utumishi tusisubiri tumestaafu ndiyo tuanze kufuatilia madai na vitu vingine, lakini pia sisi watumishi katika utumishi wetu tunatakiwa tuwe sehemu ya utatuzi wa changamoto za wananchi huko vijijini badala ya kupeleka matatizo yote kwa viongozi wa Wilaya" amesema Katibu Tawala Wilaya.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumishi waliopo makao makuu ya Halmashauri kutumia lugha chafu kwa watumishi wengine hususan waliopo vijijini ambapo amekemea vikali tabia hiyo na kuahidi kuchukua hatua kali kwa watumishi wenye tabia hizo.


Mkurugenzi Mtendaji amesikiliza kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi kupitia kikao hicho ambapo amesema kero zilizobaki ambazo zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri zitatatuliwa na zile zinazohusiana na Serikali kuu zitafikishwa kunakohusika kwa wakati.


Watumishi mbalimbali waliofika katika kikao hicho wamepongeza juhudi hizo za Mkurugenzi Mtendaji kuamua kusikiliza kero za watumishi na kuzipatia ufumbuzi papo hapo ambapo wameomba vikao kama hivyo vifanyike mara kwa mara.


Kupitia kikao hicho watumishi mbalimbali wametoa kero zao nyingi zikihusu madai mbalimbali ya uhamisho, upandishwaji wa madaraja, unadilishwaji wa miundo na maounjo ya mishahara.


Kikao kama hicho kitaendelea tena katika tarafa za Nyachenche na Katunguru ambapo watumishi wote wametakiwa kufika na kuelezea kero zao.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • WAZIRI MKUU ASIFU MAENDELEO YA SENGEREMA

    May 19, 2025
  • DED SENGEREMA AGUSWA NA KERO ZA WATUMISHI

    May 02, 2025
  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.