Jumla ya watendaji 8 wa kata za Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wamenufaika na pikipiki zilitolewa na
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa lengo kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa maofisa hao.
Akikabidhi pikipiki hizo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amewataka watendaji hao kutumia vizuri Pikipiki hizo ili ziweze kufikia malengo yalikusudiwa na Serikali ikiwemo ukusanyaji wa mapato pamoja utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
"Pikipiki hizi zimenunuliwa kwa kodi za wananchi, ni imani yangu mtazitumia vizuri tena kwa shughuli za Serikali" amesema Mhe. Ngaga.
Katika hatua nyingine Mhe. Ngaga ameliagiza jeshi la Polisi wilayani Sengerema kuhakikisha watendaji hao waliopewa Pikipiki wanapewa mafunzo ya namna bora ya utumiaji wa Pikipiki hizo na amewaagiza watendaji hao kuhakikisha wanakuwa na leseni za kutumia vyombo hivyo.
Mhe. Ngaga ameishukuru Serikali kwa kuwajali watumishi ambapo amesema ndani ya mwaka mmoja Serikali imetoa Pikipiki 83 kwa watumishi wakiwemo maafisa kilimo na watendaji wa kata za Halmashauri ya Sengerema na Buchosa
Mapema akimkaribisha Mkuu wa Wilaya kukabidhi Pikipiki hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amesema Pikipiki hizo kwa awamu hii ya kwanza zimetolewa kwa watendaji wa kata za pembezoni kwa lengo la kuwasaidia kutimiza majukumu yao ya kila siku ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Mtendaji wa kata ya Chinfunfu Emmanuel Ng'alalile ameishukuru Serikali kwa kuwasaidia usafiri ambapo amesema umbali kutoka kata hiyo hadi makao makuu ya Halmashauri ni zaidi ya kilomita 50 hivyo itamsaidia katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo upelekaji wa taarifa za ofisi pamoja na utoaji wa huduma kwa wakati.
Pikipiki hizo 8 zimekabidhiwa kwa watendaji wa kata za Chinfunfu, Igalula, Kagunga, Buyagu, Kasenyi, Buzilasoga, Igulumuki, na Ngoma.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.