Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa ngazi ya kata na vijiji wamatakiwa kuwa waadilifu pamoja na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 30,2024 na Msimamizi wa Uchaguzi wa wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Binuru Shekidele wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wasimamizi hao kuhusu mwongozo wa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Sengerema Sekondari.
Amesema iwapo wasimamizi hao watafikisha elimu sahihi kwa wapiga kura hakutakuwa na upotoshaji lakini pia wananchi wengi watajitokeza kujiandikisha ili kupiga kura kwenye uchaguzi huo.
"Katika zoezi hili ni vyema mkatoe elimu sahihi kwa wananchi, kuna uboreshaji wa daftari la wapiga kura umemalizika hivi karibuni, kwa sasa kuna zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa wananchi wenye sifa wanatakiwa wajiandikishe kwenye maeneo yao na wajitokeze pia kugombea nafasi mbalimbali, ni ninyi wa kutoa elimu hii" amesema Msimamizi wa Uchaguzi.
Wasimamizi hao pia wamekula kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Kamishna wa viapo mhe. Christopher Mbuba ambapo pia amewataka wasimamizi hao wa uchaguzi kuheshimu viapo hivyo kwani zoezi la uchaguzi ni mhimu hivyo ni vyema wasimamizi hao wakafuata miingozo kama walivyopatiwa elimu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.