Jumla ya watahiniwa elfu nane mia tano hamsini na moja. (8,551) wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Afisa Elimu wa shule za Msingi wilayani Sengerema Bwn. Oscar Kapinga amebainisha kuwa kati ya watahiniwa hao wavulana ni elfu nne mia moja thelathini na nane (4,138) na wasichana ni elfu nne mia nne kumi na tatu (4,413)
Akizungumzia suala la usimamizi wa mitihani hiyo Kapinga amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha suala la udanganyifu wa kuiba mitihani halitokei huku akiwatahadharisha wasimamizi na wanafunzi watakaofanya udanganyifu wa kuiba mitihani hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo Afisa Elimu amewataka wazazi na walezi kutowashinikiza watoto wao kufanya vibaya mtihani hiyo kwa lengo la kushindwa kuendelea na masomo yao ya sekondari hapo baadae ili wawasaidie kazi za nyumbani pamoja na kuolewa ili wapate mali.
Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi imeanza kufanyika kuanzia leo tarehe 06/09/2017 na 07/09/2017
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.