Hayo yamebainishwa leo tarehe 20 Septemba, 2023 wakati wa kikao cha kujadili mradi huo kilichowakutanisha timu ya wataalamu kutoka Halmashauri, wasimamzi wa mradi na wakandarasi wa mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ndugu Mwita Waryuba amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutoa elimu ya uhamasishaji wa jamii juu ya mradi huo, kuwajibika kwa jamii kwa kurejesha kidogo wanachokipata (CSR) na kutoa taarifa mhimu kwa uongozi wa serikali za vijiji, kata,tarafa na Halmashauri zihusuzo mradi huo.
"Mradi huu umeanza lakini hautakuwa maana kama mtashindwa kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kurudisha sehemu ya mnachokipata kwa kuwezesha baadhi ya miradi kijijini hapa" amesema ndugu Waryuba.
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi huyo amemwagiza msimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanarekebisha mapungufu yote yaliyobainika kupitia ziara hiyo pamoja na mkandarasi kuimarisha ulinzi wa eneo la mradi.
Meneja mradi huo Ombeni Justo Ikola amewaasa wananchi wafugaji wanaozunguka eneo la mradi kutokuingiza mifugo kwenye aneo la mradi ambayo inaweza hatarisha usalama wa mifugo hiyo kutokana na miundombinu iliyopo kwenye mradi huo pamoja na kukwamisha utekelezaji wa mradi huo.
Diwani wa Kata ya Katunguru Mhe. Sadick Jimola amemwomba meneja Mradi wa huo kuhakikisha taarifa za mradi zinawafikia wananchi ili kujua kinachoendelea pamoja na kuzingatia na kuungana na jamii kwenye masuala ya uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Mradi wa Umwagiliaji wa Katunguru unaojengwa na kampuni ya SIETCO na JV Jiangxi Geo- Engineering Group Cooperation kwa awamu ya kwanza utachukua Hekta 315 ambapo zaidi wakulima 600 wanatarajia kunufaika moja kwa moja na mradi huo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.