Vijana hao wamefanya maandamano ya amani ambayo yalitanguliwa na shughuli za usafi katika mji wa Sengerema maeneo ya soko kuu, ambapo lengo ikiwa ni kuunga jitihada za mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli katika utendaji wake wake wa kazi hasa jinsi anavyopambana kuhakikisha rasili mali za Taifa zinakuwa za tija kwa Taifa na watanzania wote kwa ujumla na si kwa watu wachache wasio na mapenzi mema na Taifa letu.
Akiwapokea vijana hao mhe. Mkuu wa Wilaya amewapongeza na kusema kitendo walichokifanya vijana hao ni kitendo cha kizalendo na ni kitendo amabacho kinapaswa kuigwa na jamii nzima.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.