• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Ujenzi wa Stand Mpya ya Mabasi waongeza chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Sengerema

Posted on: March 12th, 2021

Kuanzishwa kwa kituo kipya cha mabasi mjini Sengerema ambacho kitagharimu Sh100milioni hadi kukamilisha kitahudumia magari 500 kwa siku Kituo hicho kitakuwa kivutio cha uchumi kwa wakazi wa Sengerema na viongoji vyake.

Kituo hicho cha mabasi Wilayani Sengerema kilikuwa kimekwama kwa miaka kadhaa bila kukamika hatimaye kimekamilika kwa hatua ya awali na kuanza kutumika.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Magesa Mafuru amesema Kituo hicho kwa Sasa kimegharimu zaidi ya Sh 50 milioni kwa hatua za awali na hadi kitakapo kuwa kimekamilika kitagharimu zaidi ya Sh100 milioni.

Magesa amesema suala la ujenzi wa Kituo hicho ulikuwa mpango wa Halmashauri ya Sengerema tangu mwaka 2010 haukukamilika na mwaka 2016 alipoingia Halmashauri ya Sengerema baada ya kuteuliwa alianza mchakato wa kuhakikisha kituo hicho kinakamilika na  kisha kuanza kazi.

Amesema kukamika kwa Kituo hiki kipya cha mabasi Halmashauri inatarapjia kukusanya mapato ya serikali kiasi cha Sh 25milioni kwa mwezi kiasi ambacho kitaongeza mapato ya Halmashauri tofauti na zamani walikuwa wanakusanya Sh20milioni kwenye Kituo cha zamani.

Mafuru amesema Kituo hicho cha mabasi kitahudumia magari 250 kwa Sasa na kitakapo kamilika kitahudumia magari 500 kwa siku na kuongeza mapato kwa Halmashauri.

"Mpango wetu tutajenga Vituo vingine viwili vya mabasi kwenye kata ya Igalula Kijiji cha Ngoma na kata ya katunguru Kijiji cha mbalagane lengo nikuongeza mapato ya Halmashauri kutokana na Serikali kuzitaka Halmashauri kubuni vyanzo vya mapato ili ziweze kujiendesha" amesema, Magesa.

Mapato ya ndani ya Halmashauri yameongezeka kutoka Sh1.5bilioni kwa mwaka 2020/2021 hadi kufika mapato ya Sh1.7bilioni kwa mwaka 2021/ 2022 kutokana na mapitio ya kina kwa baadhi ya vyanzo mapato kuongezwa.

Ili kuongeza mapato na uchumi wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 wamejielekeza kusimaamia vyanzo vikuu vya mapato ambavyo ni Kituo kipya mabasi, mnada wa mifugo sima, Mialo ya kupokelea Samaki pamoja na kujikita katika ukusanyaji mapato kwenye chanzo cha Washereheshaji wakiweo wapiga picha, ma MC, wapishi na wapambaji.

John Njile ni mwenyekiti wa kituo cha mabasi Sengerema amesema licha ya Halmashauri hiyo kufungua stendi mpya amewataka Wamiliki wa magari na watu wanaotoa huduma kwenye Kituo hicho cha mabasi kuwa makini katika kuwahudumia Wananchi.

Aliwataka pia Madera wa magari kuacha tabia ya kupakia abiria maeneo yasiyo rasmi kwa kuwa wakifanya hivyo watakuwa wamekwenda kinyume na utaratibu.

Nao akina mama lishe wanaofanya Shughuri za kuuza vyakula kwenye kituo kipya cha mabasi mjini Sengerema wamasema kituo hicho kimekuwa kivutio kwa kufanya biashara kutokana na kupata wateja wengi tofauti na Kituo Cha zamani ambapo kuliwa na eneo dogo la kufanyia biashara.

Estar Samsoni mama lishe amesema ndani ya siku mbili tangu Kituo hicho kilipofunguliwa wanafanya biashara kubwa kwa kuuza vyakula hadi sh.50000 kwa siku na kuendesha familia zao.

Madeva wa bajaji wao wamesema wamekuwa wanapata faida kubwa ya kusafirisha abilia kuwapeleka stand mpya na  hivyo kujiongezea kipato tofauti na mwanzo.

"Kwa sasa kuanzia asubuhi hadi jioni tunakuwa tunalala na kati ya sh 50000 hadi sh100000 kiasi ambacho kwetu ni faida kubwa amabayo inatokana na kituo hicho kipya cha mabasi" alisema Solo Juma dereva bajaji.

Pia ameiomba Halmashauri kuendelea kuibuni vyanzo vipya vya mapato na kufungua uchumi wa wanasengerema kwa lengo la kujikwamu kimaisha.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole licha ya kuzindua Kituo hicho amewataka Wananchi kuchangamkia fursa la kupata maeneo ya viwanja kwenye stendi mpya ili kuinua uchumi wao.

Sambamba na hilo amepiga marufuku kufanya Udalali wa viwanja maeneo ya Stendi atakaye bainika atachukuwa Sheria.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Yanga Makaga alisema Kituo hiki kipya cha mabasi kitakuwa mkombozi kwa kuongeza mapato ya halmashauri.

Wananchi wilayani Sengerema wamefurahia suala la kuzindua kwa kituo kipya cha mabasi ambacho kitawapitia fursa ya kufanya biashara zao.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.