Halimashauri ya Sengerema katika kutekeleza mradi wa upanuzi wa Kituo cha Afya cha Kagunga unazidi kuimarika baada ya kuwa na sifa nzuri kila viongozi mbalimbali wanapotembelea kituo hicho kwa lengo la kujionea maendeleo ya mradi huo ambao mpaka sasa nyumba ya mtumishi ipo kwenye hatua ya umaliziaji huku majengo mengine yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi. Ikiwa ni jitihada za usimamizi mzuri wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa ili wananchi waweze kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.
Serikali imetoa kiasi cha sh.milion 400 kwa ajiri ya upanuzi wa kituo hicho kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi hasa wa hali ya chini ambao walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukoswa huduma ya upasuaji karibu, majengo yanayojengwa katika kituo hicho ni Chumba cha upasuaji, chumba cha kuwekea maiti, jengo la mama na motto, maabara, wodi ya wanaume na watoto pamoja na jengo la wagonjwa wa nje.
Nae Mkurugenzi mtendaji halimashauri ya Sengerema Bwn. Magesa mafuru alisema kuwa atasimamia vema miradi yote ya maendeleo katika halmashauri yake na wala asitokee mtu yoyote kujidanganya kukwamisha mradi wowote anajisumbua.
Huku Mgaga mkuu wa Halimashauri ya Sengerema Bwn. Peter Mahu alisema wako macho katika matumizi ya fedha nawatahakikisha hakuna kitu kinachopotea na majengo haya yatajengwa kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa kunausimamizi mzuri.
Mmoja wa wananchi wa kata ya Kagunga Juma Malima alisema kuwa kutokana na upanuzi huu utawasaidia kuokoa maisha yao ambayo walikuwa wakiyapoteza kutokana na kukoswa huduma mhimu hasa upasuaji na kupata vipomo sahii vya maabara na kutoa pongezi kwa serikali.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.