Mji wa Sengerema na viunga vyake limepata ufumbuzi wa kudumu kutokana na kamapuni ya STUMARCOT CO LTD ya jijini mwanza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Halimashauri ya Sengerema kwa kuzoa taka na kuhakikisha mji unakuwa katika mazingira safi muda wote.
Meneja maradi wa kampuni hiyo Flavinian Kassange amesema kuwa kampuni yao imeingia mkataba na halimashauri ya Sengerema kwa kufanya usafi katika mji huo ili kuhakikisha unakuwa safi na zoezi hilo limeanza kutekelezwa kuanzia Julay 13 mwaka huu.
Amesema kampuni hiyo imejipanga na kujidhatiti katika swala zima la ufasi wa mazingira ya mji, na kuiomba jamii nzima ya Sengerema kutoa ushirikiano wa kutosha katika swala zima la usafi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama ili kuepuka magonjwa yamlipuko hasa kipindupindu ambayo yanatokana na swala zima la uchafuzi wa mazingira.
Kassange amesema watu walioingia nao mkataba katika kufanya usafi niwale waliokuwa wanafanya kazi hizo na Halimashauri ya Sengerema hivyo matumaini yake ni kuona wanafanya kazi kwa weredi kutokana na ukweli kuwa mazingira yote mji wanayafahamu na wao kama kampuni watawajibika kuwalipastahiki zao kutokana na mikataba yao.
Nae mkuu wa idara ya Mazingira na Usafishaji Ndg. Salim A. Sallim amewaomba wananchi wa Sengerema kutotupa taka ovyo na badara yake wanatakiwa waziweka katika sehemu maalumu ambazo kuna vizimba ili iwe rahisi kwa watu wanaofanya usafi kuzikusanya na kuzipekeleka mahali husika.
Baadhi ya wananchi wa Sengerema wakitoa maoni yao juu ya swala zima la usafi wamesema kuwa ujio wa kampuni hii utasaidia kupunguza swala la uchafu katika mji wa Sengerema na tunatarajia mafanikio makubwa kwani kasi ya ufanyaji usafi wa kampuni hii ni wa hali ya juu kwani ndani ya mda huu mfupi mafanikio yanaonekana wazi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.