Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) Wilaya ya Sengerema kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema leo (31.05.2024) wamepanda miti ya kivuli aina ya Midodoma mjini Sengerema kandokando ya barabara kuu ya Sengerema-Geita ikiwa ni sehemu ya kurejesha miti iliyokatwa kimaokosa mwezi April 2024.
Akiongea wakati wa zoezi hilo, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Sengerema, Martin Kilenga amesema wameamua kupanda miti hiyo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi pamoja viongozi wa Wilaya hivyo wameona ni vyema kupanda miti hiyo na kuahidi kuitunza kwa siku zote kwa kushirikiana na wafanyabishara.
"Sisi kama TANESCO tunajali sana mazingira, na hii miti ndo vyanzo vya kuhifadhi mazingira yetu, na inaleta maji ambayo yatakwenda kwenye mabwawa na ndo tunapata umeme huu tunaoutumia" amesema meneja wa TANESCO.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Ally Salim amesema miti iliyokatwa tayari ilianza kuleta vivuli pembezoni mwa barabara kuu hivyo wameona ni vyema kupanda tena miti mingine ili kurudishia vivuli vilivyopotea na amesema wanapanda miti aina ya Midodoma ambayo ni stahimilivu na inakuwa kwa haraka ambapo amewaomba wafanyabiashara na wajasiriliamali wanaofanya biashara zao pembezoni mwa barabara kuhakikisha wanaitunza vizuri miti liyokatwa na baade kuchipuka tena kwani watanufaika zaidi na miti hiyo.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia zoezi hilo wamesema wamefurahi kuona TANESCO wamechukua hatua ya kupanda tena miti hiyo ambapo wamesema kitendo hicho ni cha kiungwana na wameahidi kuilinda kwani tayari walishaona manufaa ya kuwa na miti kandokando ya barabara kuu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.