Zahanati ya Sima iliyopo kata ya Sima Wilayani Sengerema imeongoza kwenye zoezi la utoaji wa chanjo kwa njia ya Mkoba (outreach services) kikiwa ni miongoni mwa vituo vilivyofanyiwa usimamizi shirikishi na timu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wizara ya afya kwa kipindi cha Januari hadi Julai 2023.
Mbali na utoaji wa Chanjo kwa njia ya Mkoba, Zahanati hiyo pia imeongoza kwa utunzaji wa nyaraka za kituo pamoja na ukamilishaji wa huduma za Mkoba kama zilivyopangwa kwenye ratiba ya kila mwezi.
Akitoa pongezi hizo leo Jumatatu Agosti 14, 2023 kituoni hapo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Dkt. Fredrick Mugarula amepongeza uongozi wa Zahati hiyo kwa kufanya vizuri katika utoaji wa huduma hizo za afya umakini na kuwataka watumishi wa kituo hicho kuendeleza jitihada hizo bila kuchoka.
"Zahanati hii mmefanya vizuri, ni vizuri na sisi tuwape pongezi kama Halmashauri ili iwe kumbukumbu yenu, tunatambua vyema jitihada zenu" alisema Mganga mkuu wakati akikabidhi cheti cha pongezi kituoni hapo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya ya watumishi wa Zahanati hiyo, Mganga mfawidhi wa Zahanati hiyo Amos Bombot amesema Zahati ya Sima imefanya vizuri kwenye huduma za Chanjo kutokana na kupeleka huduma za Chanjo moja kwa moja kwa walengwa ambapo wamekuwa wakifika katika ngazi ya vitongoji pasipo kuwasubiri walengwa kufika kituoni hapo ambapo amesema huduma hizo zimekuwa zikitolewa kwa ushirikiano mkubwa uliopo baina ya watumishi na viongozi wa serikali za vijiji vya Ishishang'olo na Sima.
Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Bi. Mageni Magesa amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ina vituo 48 vya kutolea huduma za Chanjo ambavyo vyote vimekuwa vikitoa huduma bora za Chanjo kwa njia ya Mkobaa na kwa wakati.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.