Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amezitaka shule za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuhakikisha zinashirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali ya kitaaluma kujifunza kutoka kwa shule zinazofanya vizuri ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Mkurugenzi Mtendaji ameyasema hayo wakati wa hafla ya kupokea matokeo ya mtihani wa kumaliza nwaka 2022 kwa kidato cha kwanza na cha tatu kwa shule za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mtihani ambao umekuwa ukifanyika kila mwaka na kusimamiwa kwa Umoja wa Wakuu wa Shule (TAHOSA).
Mkurugenzi Mtendaji amesema kuna baadhi ya shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema imekuwa zikifanya vizuri kitaaluma na zingine zimekuwa zikifanya vibaya kila mwaka hivyo amewaagiza wakuu hao wa shule kuweka mipango mizuri ili kuondokana na matokeo mabaya kwa wanafunzi.
"Tuone namna nzuri ya kusaidiana kwenye baadhi ya masomo, kwanini shule zinazofanya vizuri ni zilezile na zinazifanya vibaya pia ni zilezile, tuchukue hatua tubadilke tunaweza na zile shule zinazofanya vibaya tutaziweka kwenye uangalizi maalumu"
Mwenyekiti wa kamati ya taaluma ya TAHOSA Mwalimu Christine Zegera akiwasilisha matokeo hayo amesema miongoni mwa changamoto zilizojitokeza katika kufanikisha mtihani huo ni pamoja na gharama ndogo za uendeshaji wa mtihani huo ukilinganisha na hali halisi ya gharama za maisha kwa sasa ambapo kumesababisha kamati ya maandalizi kushindwa kukidhi mahitaji ya huduma kwa walimu hasa kwa wale wanaotoka mbali na vituo vya kazi kupata chakula na malazi.
Mwenyekiti huyo amependekeza kwa mwaka ujao kila mtahiniwa achangiwe kiasi cha shilingi 5500 ili kukidhi gharama za uendeshaji wa mitihani hiyo.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Sekondari Amani Tangalo amesema kufanyika kwa mtihani huo inasaidia Halmashauri kuweza kujua ni maeneo yapi yawekewe mkazo zaidi na walimu na pia husaidia kupata picha halisi ya matokeo ya kidato cha pili na nne kwa mwaka unaofuata hivyo amewataka wakuu wa shule kuhakikisha wanakuwa na mikakati thabiti ili kuboresha taaluma katika shule husika.
Mtihani huo wa pamoja hufanyika kila mwaka ambapo hushirikisha kidato cha kwanza na cha tatu. Kwa mwaka huu jumla ya shule za Sekondari 40 zineshiriki katika mtihani huo kwa kidato cha kwanza na shule 38 zilishiriki kwa mtihani wa kidato cha tatu.
Katika matokeo hayo Seminari ya Sengerema Imeongoza katika shule 40 kwa kidato cha kwanza kwa kupata wastani wa alama 69.9 na shule ya Twitange imeongoza kwa kidato cha tatu katika shule 38 kwa kupata wastani wa
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.