Akizungumza ndani ya kikao cha uzinduzi kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo FDC Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw. Emily Kasaga amesema kuwa “Mkoa wa mwanza ni mojawapo ya mikoa ya kanda ya ziwa yenye vifo vingi vya watoto wachanga ambapo mwaka 2020 Mkoa ulikuwa na jumla ya vifo 837 sawa na vifo 6 Kati ya vizazi hai 1000”
Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa mwanza Emili Kasaga wakati wa uzinduzi wa mpango wa matibabu kwa njia ya uwiano kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyika Wilayani Sengerema Mkoa wa mwanza.
Pia amesema kuwa vifo vya watoto 67 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa bado hai na vifo 43 vya watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa hai bado ni vingi huku Mkoa wa mwanza ukitajwa kuwa na vifo vingi zaidi, Kati ya vifo hivyo vya watoto wachanga 118 (0-28) sawa vifo 5 Kati ya vizazi 1000 vilitokea Halmashauri ya Sengerema.
Brandina Hezron Msaidizi mratibu wa Afya ya mama na mtoto wilaya ya Sengerema amesema sababu ya vifo vya watoto hao ni kuwa na uzito pungufu, kushindwa kupumua na uambukizo wa magonjwa mbalimbali.
Mwakilishi mkazi wa Shirika lisilolakiserikali la PATH nchi Tanzania Amos Mugisha amesema kutokana na vifo vingi vya watoto Wilayani Sengerema Shirika hilo likishirikiana na Serikali limekuja na mpango wa kukabiliana na changamoto hiyo.
Mradi huyo utafanyika kwenye Vituo vya afya vitano, na zahanati 29 ambapo wametoa vifaa vya utambuzi wa oxjen kwa mtoto pamojana vifaa vya utambuzi wa ndani ya mtoto.
Mganga mkuu wa Mkoa wa mwanza Thomas Ruta amesema mradi huu wameupokea kwa mikoano miwili na utatekezwa kwa ufanisi mkubwa ili kuokoa vifo vya mama na mtoto.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Salim Ally, akitoa neno la shukurani amesema kuwa yeye kama msimamizi wa mkuu atahakikisha mradi huu wa utoaji wa huduma ya matibabu kwa watoto kwa njia ya uwiano unafikia malengo hivyo kila mmoja katika maeneo yake ya kazi ajitahidi kuhakikisha anatimiza wajibu wake hasa katika vituo vya afya pamoja na zahanati zinazopatikana katika wilaya ya Sengerema.
Pia amewashukuru viongozi toka shirika la PATH kwa jinsi walivyoguswa na changamoto ya vifo vya watoto na kuja na mpango wa kunusuru vifo vya watoto kupitia mpango wao wa matibabu kwa njia ya uwiano.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.