Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza imeadhimisha sehere za miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kupanda miti na kufanya usafi kwenye hospitali ya Wilaya Mwabaluhi na Kituo cha Afya Sengerema.
Akiongoza zoezi la upandaji miti 500 katika eneo la shule mpya ya Sekondari Isungang’holo, Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Curthbert Midala, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao kwani kupanda miti kuna faida nyingi ikiwemo kutunza mazingira pamoja na matunda.
"upandaji wa miti una faida nyingi sana, ikiwemo kivuli, mbao, upatikanaji wa matunda.., zoezi hili ni la mhimu kweli na kila mmoja aone kuwa anao wajibu wa kuitunza" amesema Katibu Tawala Wilaya.
Kwa upande wake Afisa mazingira Halmashauri ya Sengerema Bi.Tandy Laizer amesema jumla ya miti 500 imepandwa katika eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari isungang’holo ikiwemo miti ya matunda, mbao na vivulli.
Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema , Wilbard Bandola amewashukuru wananchi kujitokeza kuazimisha miaka 63 ya uhuru kwa kupanda miti eneo hilo hivyo amewaomba wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo kuhakikisha wanailinda.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isungang’holo, Michael Sumuni pamoja na wananchi wamewashukuru viongozi wa halmashauri ya Sengerema kwa kuamua kufanyia maadhimisho hayo katika eneo la shule mpya pamoja na kupanda miti hiyo ambapo wameahidi kuitunza.
Miti iliyopandwa leo imetolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzaniaa (TFS) wilaya ya Sengerema lengo ikiwa ni uhifandhi wa mazingira kwa njia ya kupanda miti.
Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka 2024 yameadhimishwa kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo usafi na upandaji wa miti. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.