Wakazi Sengerema mkoani Mwanza watanufaika na ujenzi wa Barabara ya lami kutoka Sengerema hadi Nyehunge yenye urefu wa kilomita 54.4 na ujenzi wa Kivuko kipya kitakachounganisha wakazi wa Buyagu Wilayani Sengerema na Mbalika wilayani Misungwi.
Hayo yamebainishwa leo mjini Sengerema wakati wa Hafla ya utiaji saini kati Serikali na kampuni ya AVM-Dilingham ya nchini Uturuki itakayojenga Barabara hiyo kwa gharama ya shilingi 73.04 bilioni kwa muda wa miezi 28 na ujenzi wa kivuko kipya cha Buyagu-Mbalika kwa gharama ya shilingi 3,817,064,000 kitakachojengwa na kampuni ya Songoro Marine kwa muda wa miezi 10.
Akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji saini, Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Godfrey Kasekenya amewataka wananchi wanaozunguka Barabara hiyo kuepuka vitendo vya uhalifu wa namna yoyote kwa vifaa vya ujenzi nabadala yake amewataka wavilinde.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroad, Rogatus Mativila amesema kukamilika kwa ujenzi wa Barabara hiyo kutachochea shughuli za mbalimbali za kiuchumi na itaunganisha mikoa ya kanda ya ziwa hivyo.
“Kukamilika kwa Barabara hii kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa mazao ya misitu, mazao ya chakula, mazao ya uvuvi pamoja na mazao ya biashara na shughuli zingine za kijamii" amesema mtendaji mkuu wa TANROAD.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala amesema kukamilika kwa ujenzi wa kivuko cha Buyagu-Mbalika kutataondoa kero nyingi za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo hivyo kukamilika kwake kutasaidia shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii.
Mbunge wa jimbo la Sengerema, Mhe. Hamis Tabasamu amesema kujengwa kwa barabara hiyo kutasaidia kuleta fursa nyingi kwa wakazi wa Sengerema na Buchosa hivyo amewataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanailinda vyema miundombinu ya Barabara hiyo pamoja vifaa vya ujenzi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.