Shule za Sekondari za Kijuka na Katuguru zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza zimepongezwa kwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne 2023 ambapo.
Akitoa pongezi hizo leo Oktoba 1, 2024 mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bi. Genoveva Chuchuba amesema pongezi hizo zimetolewa kufuatia tuzo zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ilifanikiwa kupata tuzo kadhaa ikiwemo ya mshindi wa pili miongoni mwa Halmashauri nane za mkoa wa Mwanza kwenye matokeo ya kidato cha nne 2023.
"Nimekuja kuwapongeza, matokeo haya yamekuja kutokana na jitihada zenu, ushirikiano wenu na juhudi za kila mmoja wenu" amesema Bi. Chuchuba.
Katika tuzo hizo ya shule ya Sekondari Kijuka imepata cheti cha pongezi kuyoka kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kutokana na maendeleo chanya ya kitaaluma ya shule kwa miaka miwili mfulukizo ambapo imefanikiwa kupandisha ufaulu kwenye matokeo ya kidato cha nne 2023.
Sekondari ya Katunguru ambayo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kwenye matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo na kufanikiwa kuwa miongoni mwa shule kumi bora kwa mkoa wa Mwanza.
Katika tuzo zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza hivi karibuni, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kupitia divisheni ya Elimu Sekondari ilifanikiwa kupata jumla ya tuzo 4, ikiwemo ya mshindi wa tatu kwenye mtihani wa kidato 2023, mshindi wa tatu kwenye mtihani wa kidato cha 2023, mshindi wa tatu kwa mtihani wa kidato vha sita 2023 na tuzo ya Halmashauri bora iliyofanikiwa kupandisha ufaulu zaidi katika matokeo ya kidato cha nne 2023.
Katika tuzo hizo walimu wawili wa masomo ya Kemia na Kiingereza kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema waliibuka walimu bora na kupewa zawadi ya fedha.
Wakishukuru kwa pongezi hizo Mkuu wa Sekondari ya Kijuka Mwalimu Patrick Juvenali na Mkuu wa Sekondari ya Katunguru Mwalimu Baraka Msimba wameushukuru uongozi wa Halmshauri kwa pongezi pamoja na zawadi ya keki wakisema kuwa kitendo hicho kimewapa moyo na kinaenda kuwa kichocheo cha wao kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya kitaifa.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.