Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza imedhamiria kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto zaidi ya 3000 wenye umri wa kuanzia miaka 14.
Afisa afya wa halmashauri hiyo Bwn.Wilbod Mayumbu ambaye alimwakilishwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Dk. Peter Mahu wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika katika kituo cha afya Katunguru, alisema kuwa walengwa katika chanjo hiyo ni wasichana waliopo shuleni pamoja na wale ambao hawasomi waliofikisha umri kuanzia miaka 14 hadi 19
Dkt. Angelina William Samike Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika uzinduzi huo ameitaka jamii kuwaruhusu watoto na walengwa wote wa chanjo kujitokeza katika zoezi hilo kwa kuwa halina madhara yoyote, huku akibainisha chanzo kikuu cha Saratani ya mlango wa kizazi ni kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo, pia kuwa na wapenzi wengi, kupata mimba katika umri mdogo pamoja na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Aidha uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi umeambatana na uzinduzi wa chanjo ya ugonjwa wa kupooza inayotolewa kwa watoto wote wa kuanzia wiki kumi na nne.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.