Kuanzishwa kwa mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS *(Public Employee Performance Management Information Sysytem)* na PIPMIS *(Public Institutions Management Information Sysytem)* utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma pamoja na kuondoa hisia za upendeleo na uonevu katika tathimini ya utendaji kazi uliokuwa katika mifumo ya awali ya OPRAS na IPCS.
Hayo yamebainishwa leo Disemba 07, 2023 wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa watumishi Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.
Akitoa Mafunzo hayo Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Ndugu Rwechungura Mtalemwa amesema kuanzishwa kwa mfumo wa PEPMIS na PIPMIS kutasaidia kondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika mifumo ya OPRAS na IPCS iliyokuwa ikitumika hapo awali hivyo amewataka watumishi wa umma kuulewa vizuri mfumo huo.
Ndugu Mtalemwa ameongeza kusema kuwa mifumo hiyo ya awali haikuakisi hali halisi ya utendaji kazi wa watumishi ambayo ilihusishwa na upendeleo au uonevu kwa baadhi ya watumishi na viongozi katika baadhi ya taasisi.
"Mifumo hii haikuwa na uwezo wa kutoa taarifa za utendaji kazi wa watumishi na taasisi kwa siku, wiki au mwezi lakini pia haikuweza kupima uwajibikaji na uwajibishaji watumishi na taasisi za umma lakini mfumo mpya unaweza na umezingatia na utapima uwajibikaji wetu" ameongeza kusema Ndugu Mtalemwa.
Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkurugenzj Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Ndugu Wilbard Bandola mewataka watumishi wa umma kuzingatia mafunzo hayo na badae waweze kutoa elimu kwa watumishi wengiwe waliopo chini yao.
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala, Christina Bunini amesema kupitia mfumo huo watumishi wa Umma sasa watapimwa utendaji kazi kupitia mfumo huo hivyo amewataka watumishi hao kuzingatia vyema mafunzo hayo ili badae waweze kuingiza taarifa za utendaji wao kwa usahihi sambamba na kutoa elimu kwa watumishi wengine.
Mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma umesanifiwa ili kutatua chamgamoto za mifumo ya OPRAS na IPCS ambayo imesitishwa mwaka 2022 na utatumika katika taasisi zote za Serikali.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.