Mhe Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto atembelea Zahanati ya Nyamizeze wilayani Sengerema kwa lengo la kujiridhisha na uhalali wake baada ya kupata Nyota Nne katika mpango wa lipa kwa ufanisi katika mkoa wa Mwanza (P4R) na kutoa cheti alipofanya ziara yake ya kikazi Julai 17 mwaka 2018
Katika ziara hiyo Mhe. Faustine Ndungulile ameipongeza timu nzima ya zahanati ya Nyamizeze kwa njinsi inavyofanya kazi yake vizuri na kusema ameridhishwa na hadhi iliyopatiwa kwani katika maeneo yote aliyotaka kujiridhishwa Zahanati hiyo imefanya vizuri zaidi ya alivyokuwa akidhania.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa kituo hicho; akitoa neno kwa Mhe Naibu Waziri Dr. Ndungulile Bi. Zuhura amesema siri ya mafanikio yote hayo ni kufanya kazi kama timu moja jambo ambalo linakifanya kituo cha cha Zahanati yao kufanya vizuri kwani kila mmoja anashiriki.
Katika hatua nyingingine Dr. Ndungulile alipata fursa ya kuona shughuli zinazofanywa na shirika la (JSI) katika Hospitali Teule ya DDH ambalo linajishughulisha na utoaji wa huduma za afya ngazi ya jamii na baadae kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa hospital hiyo amewahasa kutoa huduma zilizo bora na kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa kipindi tunapowapa huduma za matibabu, alisisitiza kwa kusema “mgonjwa anahitaji kufarijiwa na kutiwa moyo”
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Bw. Magesa Mafulu alipokuwa akitoa shukrani zake kwa Mhe. Naibu Waziri wa Afya amemwahidi kufanyia kazi maelekezo pamoja na maagizo yote aliyowapatia.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mwl. Enock Kipole akitoa salamu zake kwa Naibu Waziri Dr. Ndungulile amemshukuru yeye binafsi kwa juhudi zake anazozifanya katika kuhakikisha jamii nzima nchini Tanzania inapata huduma bora za afya jambo ambalo sasa kila mmoja ni shahidi na anaona matunda ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya kiongozi wake Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.