Mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Mhe. Emmanuel Kipole amezitaka Kamata hizo kuhakikisha zinatumia madawa waliyopewa na Seikali bure kama chachu ilikujipanga kujiendesha zenyewe siku za usoni bila kutegemea tena madawa kutoka serikalini.
Akikabidhi dawa hizo katika kamati ya Josho la Rwenge, alisema kuwa, " sasa umefika wakati wa kila mmoja wetu kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuhakikisha dawa hizi hakuna mjanja mjanja yeyote anayeziiba" pia amewaomba wananchi wanaojishughulisha na ufugaji kufata maelekezo ya wataalamu ili kuleta tija katika sekta ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kuzingatia gharama za tozo kwa kila mfugo ambapo ng'ombe ni shilingi 50 na mbuzi shilingi 25 tu.
Nae Mtendaji wa Kata hiyo akipokea dawa hizo kwa niaba ya Serikali ya kata amemwahidi mkuu wa wilaya kuwa maelekezo yote aliyoyatoa watayazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama na ulinzi wa dawa hizo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.