Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mongella ameupongeza uongozi na Halmashauri ya Sengerema kwa namna ambavyo wameweza kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo, ameyasema hayo alipokuwa ziarani katika Halmashauri ya Sengerema, katika kituo cha Zahanati ya Kasenyi ambapo kulikuwa na mradi wa wodi ya wazazi ambao kimsingi Mhe. Dr. John Pombe Magufuli alitoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya maboresho ya Zahanati hiyo.
Ndipo uongozi ulipoamua kuanzisha ujenzi wa wodi wa wazazi ili kuleta tija zaidi hasa kwa akina mama ambao walikuwa wanapata shida kubwa wanapofika kujifungua kituoni hapo, hata hivyo sasa ujenzi wa Wodi hiyo umekamilika na akina mama wanafurahi hduma bora katika kituo hicho.
Mkuu wa mkoa amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kuwa na watoto wa kutosha kwani Serikali imeamua kuboresha huduma kwa jamii hivyo hakuna mtoto anayeweza kupata shida na ndiyo maana serikali imeamua kutoa Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Pia alipata fursa ya kukagua maendeleo ya mradi wa Maji Nyampande ambao unatakiwa kukamikika ifikapo Juni 2020 akipokea taarifa hiyo toka kwa kaimu Mkurugenzi wa MWAUWASA amewaangiza kuhakikisha maji yanatoka ifikapo Januari 2020 kwani hakuna sababu ya msingi kufanya mradi uchelewe ili hali pesa ipo hivyo ameutaka uongozi kuhakikisha unamsimamia mkandalasi anafanya kazi usiku na mchana ili mradi ukamilike mapema zaidi.
Na mwisho amesisitiza watu kutumia fursa hii ya zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya kufanya chaguzi za viongozi wa Serikali za Mitaa ifikapo novemba 24 2019
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.