Wanachi wilayani Sengerema wamefurika sehemu mbalimbali kuangalia uwasirishwaji wa Riporti ya pili ya kamati maalumu iliyokuwa ikichunguza mdini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini yaliyopo sehemu mbalimbali hapa nchini na kutoa maoni mbalimbali juu swala hilo na kuitaka serikali kuchukuwa hatua dhidi ya wote waliosabisha hasara kwaTaifa letu.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Sengerema Ndg. Magesa Mafuru amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo katika nchi na tumsaidie Raisi katika vita ya kupambana na swala la watu wachache ambao wamehujumu inchi yetu katika swala zima la mikataba ya madini na kuhalalisha rasilimali za Taifa kupolwa na watu wachache.
Jaji Tasinga ni mwanachi wilayani sengerema aliyekuwa akifuatilia swala zima la uwasilishwaji wa ripoti hiyo yeye amesema kuwa katika swala zima la kuhakikisha mambo haya yanakwisha ni jukumu la chombo cha kutunga sheria ‘bunge kutengua na kubadilisha sheria ya mikataba ya madini kwa kuwa wao ndiyo waliyotunga hivyo hakuna chombo kingine cha sheria kitakacho fanya hivyo na kuwataka wabunge katika hili wanapaswa kuwa wazalendo na kuanagalia upya mikataba ili ilete tija kwa watanzania wote katika kunufaika na rasilimalim za nchi yao.
Alex Ramadhan ni mtumushi wa halmashauri ya Sengerema amesema kuwa kwanza anapongeza jutihada zilizofanywa na mkurugenzi wa halimashauri ya Sengerema kujumuika na watumishi na wananchi kwa ujmla kuangali uwasilishwaji wa ripoti na kusema kuwa mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo yanapaswa kufanyiwa kazi kwa kuwa yamegusa maisha ya watanzania na kuitwa masikini huku taifa letu ni tajiri hivyo kama mapendekezo hayo yatafanyiwa kazi basi dhahili watanzania tutakuwa watu ambao siyo ombaomba.
Dkt Agerina Samike yeye amesema kuwa kutokana na ripoti hii imeonyesha wazi kuwa tatizo ni chombo cha kutunga sheria, wabunge, kwani pamoja na wanasheria wa nchi kukubali kupitisha sheria ambazo hazina tija kwa taifa hivyo wabunge wote kwa pamoja hawana budi kutengue sheria hizo na kujadili upya ili zilete manufaa kwa ya wantanznia wote.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.