Ndg. Magesa Mafuru amemkabidhi zawadi Rosemary Benjamini aliyekuwa anasoma katika shule ya Sekondari Kilabela iliyopo kata ya Nyatukala katika Halimashauri ya Sengerema mkoani Mwanza, baada ya kuingia kumi bora kwa wasichana katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2014 kwa kufanya vizuri kitaifa katika somo la Fizikia kwa kupata alama [A] katika somo la Fizikia.
Akitoa zawadi hiyo ya simu aina ya Huwawei (Tablet) iliyotolewa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi kwa lengo la kumtia moyo, Amesema kuwa mwanafunzi huyu ameitoa kimasomaso Halimashauri ya Sengerema , na wilaya kwa ujumla kwa kuingia kumi bora katika somo la sayansi hivyo ni jambo la kujisifia na kuwataka wasichana wakaze uzi katika swala zima la kusoma ili kundesha maisha yao ya baadaye.
Magesa amemwelezea mwanafunzi huyo kuwa ni mfano wa kuigwa hivyo anamtaka akazane na kujiwekea malengo ya kufauru vizuri katika safariyake ya masomo hadi atakapo hitimu masomo yake ya elimu ya juu.
Kwa upande wake Rosemary Benjamini amesema kuwa siri ya mafaniko yake ni kujituma katika masomo kwa kujisomea mara kwa mara na kujipangia ratiba yake vizuri ya kila siku na kujiepusha na vishawishi visivyo vya lazima hivyo amewataka wasichana wenzake wajitahidi katika masomo ili waweze kufaulu katika masomo yao, huku akisema baada ya kumaliza masomo yake lengo lake ni kuwa Daktari wa binadamu.
Nae Makamu Mkuu wa shule ya Sekondary Kalabela Winstoni Kalugura ambaye alikuwa ni mwalimu wake wa somo la Fizikia amesema mwanafunzi huyo anastahili kupata zawadi hiyo kwa kuwa alikuwa anajituma katika masomo yake na alionyesha juhudi hizo akiwa tangu kidato cha kwanza.
Amabapo Kaimu afisa Elimu Sekondary Halimsahauri ya Sengerema Ndg. Aman Tangolo amesema kuwa wanafunzi wanapaswa kuwa na juhudi katika masomo ili kupata ufauru katika masomo yao na siri ya mafanikio ni kuwa na juhudi katika masomo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.