Bi. Ashura Kajuna ambaye ni Afisa Uchaguzi amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Ndg. Binuru Shekidele katika kuwaongoza mamia ya wakazi wa Sengerema katika maadhimisho ya Siku ya Magonjwa yasiyo ambukizwa kama Magonjwa ya Moyo, Kansa, Figo, Mapafu na mengine kwa kuwaasa kubadili mtindo wa maisha kama kauli mbiu inavyosema, " Badiri mtindo wa maisha kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa"
Bi Kajuna amewataka wakazi wa mji wa Sengerema kuzingatia mlo sahihi na kuacha tabia ya kula vyakula vinavyoweza kusababisha kupata magonjwa yasiyo ambukiza kama magonjwa ya moyo, huku akiwaasa vijana kupima afya zao kabla ya kufunga ndoa na wenza wao lengo ikiwa ni kutambua na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama selemundo na mengineyo.
Nae mratibu wa mgonjwa yasiyo ya kuambukiza Dr. Nelson Mtabilwa ameiomba jamii kuzingatia mazoezi ili kuepukana na kuwa na uzito uliopitiza kwani tafiti zinaonyesha magonjwa mengi husababishwa uzito uliopitiliza magonjwa hayo ni kama magonjwa ya moyo
Mganga Mkuu wa Halmashauri amewataka wananchi na wakazi wa Sengerema kuchangamkia fursa ya kupima magonjwa yasiyo ambukiza katika mabanda yaliyopo katika viwanja vya stand ya zamani ya mabasi mjini kati Sengerema kwani vipimo hivyo vinatolewa bure bila gharama zozote.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.