Imefahamika kuwa moja ya sababu ya ongezeko la maambukizi mapya ya VVU katika maeneo ya kambi za wavuvi ni pamoja na wavuvi kuhama mara kwa mara katika shughuli zao za kujitaftia kipato.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na watafiti kutoka shirika la utafiti la MITU lililopo jijini Mwanza wakati wakiwasilisha mrejesho wa matokeo ya utafiti wa Mifumo ya Mizunguzuko na wezekano wa kuwafuatilia Wanawake waliopo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya UKIMWI katika jamiii za wavuvi za ziwa Viktoria.
Mtafiti kutoka Shirika la MITU Dkt. Elialilia Okero amesema utafiti huo umefanyika katika mialo ya Igombe na Kijiweni iliyopo Manispaa ya Ilemela, Kijiweni na Itabagumba iliyopo Wilaya ya Sengerema ambapo amesema kuwa, jamii zinazoishi kandokando mwa ziwa Viktoria zina viwango vya juu vya maambukizi ya VVU hususan wanawake wanaofanya kazi katika hoteli, baa na sehemu za burudani.
Akiwasilisha mrejesho wa utafiti huo, Mtafiti kutoka shirika hilo Bi.Onike Mcharo amesema lengo kuu la Utafiti huo ilkuwa ni kufahamu mizunguko miongoni mwa wanawake wanaoishi na kufanya kazi katika jamii za wavuvi na kutathmini kukubalika na uwezekano wa kuwafuatilia katika mipango ya kuzuia na utioaji wa huduma za VVU kwa siku zijazo.
Amesema katika Utafiti huo wamebaini kuwa wanawake wenye umri mdogo (15-24) wana mizunguko mingi na mirefu ukilinganisha na wale wenye umri mkubwa.
Bi. Mcharo ameongeza kusema kufahamu namna ya mitandao inavyoathiri mizunguko ya wanawake na hatari za VVU inaweza kusaidia katika kutengeneza afua za kuzuia VVU ambazo zimeundwa kukidhi mahitaji ya watu wanaofanya mizunguko kwenye jamii za wavuvi zilizopo kwenye ziwa Viktoria.
Mrejesho wa Utafiti huo uliwashirika baadhi ya wataalamu na viongozi wa wananchi, watendaji kutoka Halmashauri za Wilaya ya Sengerema na Buchosa
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.