Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amesema uwepo wa miuondombinu bora na ya kisasa kwenye shule za Sekondari za Sengerema kunaiafanya Wilaya ya Sengerema kuwapokea wanafunzi wote 720 wa kidato cha tano waliopangiwa Wilayani hapa na njia pekee ya kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa miundombinu hiyo ni pamoja na wanafunzi hao kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo siku ya Ijumaa agosti 18, 2023 kwenye hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha tano waliopangiwa Wilayani Sengerema iliyofanyika shule ya Sekondari Sengerema.
Mkuu wa Wilaya amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya Maendeleo hususan kwenye sekta ya elimu hivyo amesema namna pekee na nzuri ya kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.
"Ndani ya miaka miwili Wilaya ya Sengerema tumepokea fedha zaidi ya bilioni 10 kwenye sekta ya elimu, haya yote yanafanyika ili kuwatengenezea mazingira mazuri ninyi wanafunzi, na njia pekee ya kumshukuru Mhe. Rais ni ninyi kupata divisheni one nyingi kweye mihani wa kidato cha sita" amesema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema amesema kufuatia matokeo mazuri ya kidato cha sita 2023, yameifanya shule ya Sekondari Sengerema kuwa ni shule ya mfano mkoani Mwanza hivyo amewaandoa hofu wanafunzi waliopangiwa shuleni hapo na Nyampulukano Sekondari kuripoti kwa wakati kwani shule zinao walimu wazuri na miundombinu bora ya kufundishia na kujifunzia hivyo hakuna sababu ya wanafunzi hao kutokufaulu vizuri.
Ndugu Shaban Lupogo mmoja ya wazazi aliyesindikiza mwanafunzi aliyepangiwa shuleni hapo kutoka Mkoani Rukwa amesifu ubora wa miundombinu iliyopo shule Sekondari Sengerema ambapo amewaomba wanafunzi waliopangiwa shuleni hapo kuhakikisha wanaripoti kwa wakati kwani shule hiyo inayo mandhari mazuri na amesifu ufaulu mzuri wa shule hiyo.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Bi. Genoveva Chuchuba amesema kwa Halmashauri ya Sengerema kati ya wanafunzi 592 waliopangiwa katika shule za Sengerema na Nyampulukano hadi kufikia siku ya Ijumaa Agosti 18, 2023 zaidi ya wanafunzi 335 sawa na asilimia 56 wameripoti katika shule hizo.
Jumla ya wanafunzi 720 wamepangiwa kujiunga kidato cha tano kupitia shule za Sengerema na Nyampulukano zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Nyehunge iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa hadi kufikia Ijumaa agosti 18, 2023 jumla ya wanafunzi 393 sawa na asilimia 54.5 wameripoti katika shule hizo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.