Halmashauri ya wilaya ya Sengerema ni miongoni mwa Halmashauri zilizopo katika nchi ya Tanzania ambayo inapatikana mkoani Mwanza katika kuhakikisha inatekeleza maelekezo, miongozo na sheria za nchi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 imeweza kutoa kiasi cha Sh. 62,400,000 ikiwa ni asilimia 39 ya bajeti ya Halmashauri ya Sh. Bilioni 1.6 toka mapato ya ndani.
Vikundi vilivyonufaika na fedha hizo ni; Wanawake Sh. 46,900,000; Vijana Sh. 12,000,000 na Walemavu kiasi cha Sh. 3,500,000
Akizungumzia mfanikio yaliyopatikana kutokana na utoaji wa fedha hizo Afisa Vijana wa wilaya Bw. Johnson, amesema makundi haya yameweza kujiendeleza kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuacha kuwa tegemezi ndani ya familia zao kwani sasa hivi vijana wanauwezo wa kujipatia kipato chao na si ombaomba kama ilivyokuwa huko nyuma akitoa mfano wa moja ya kikundi kilichonufaika na fedha hizo ni Kikundi cha Umoja wa Vijana Geita Road ambacho kinajishughulisha na shughuli za uchomeleaji.
Kwa upande wa vikundi vya wanawake tumetoa mikopo kwa vikundi zaidi ya 34 ambavyo vimepokea fedha kiasi cha Sh. 46,900,00 toka mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na Baraka Group ambacho kinapatikana Ibisabageni kinavchojishughulisha na uuzaji Vitenge, utengenezaji wa Unga wa Lishe kwa upande wake walipewa kiasi cha Sh. 1,000,000 na kimeweza kurejesha kiasi chote.
Pia kikundi cha Mwanga Group ambacho kinajishughulisha na Ufugaji wa Kuku kilipewa kiasi cha Sh. 2,000,000 na kimefanikiwa kurejesha fedha yote hivyo kimeweza kufika malengo yake na kwa sasa kinajiendesha chenyewe bila kuwa na mkopo toka Halmashauri.
Katika kundi la watu wenye Ulemavu wao wamepokea kiasi cha Sh. 3,500,000 na baadhi ya vikundi vilivyopokea fedha hizo ni Wanawake Walemavu ambacho kinajishughulisha na ushonaji wa Nguo kinachopatikana Nyatukala, kimepokea kiasi cha Sh. 1,000,000 na kimeweza kurejesha Sh. 600,000
Heldep Group ni kikundi kinachopatikana Ibisabageni kinachojishughulisha na utengenezaji wa Viatu kilipokea kiasi cha Sh. 1,000,000 na kimerejesha Sh. 700,000
Katika kutekeleza sheria hii ambayo inazitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha inatoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya makundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu, Halmashsuri ya Sengerema imekuwa ikikutana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na;
Mosi maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali ambayo hupelekea utekelezaji wa bajeti kuwa mgumu kwani yamekuwa yakiingilia shughuli za utekelezaji wa bajeti husika hasa katika bajeti ya makusanyo ya ndani.
Marejesho ya mikopo kutorejeshwa kwa wakati toka kwa makundi yaliyokopa hivyo kupelekea ule mzunguko wa kuweza kukopeshwa na makundi mengine kuwa mgumu.
Kusambaratika kwa makundi haya hasa vijana ambao wengi wao wamekuwa ni watafutaji wa maisha na hivyo hivyo kupelekea makundi haya kusambaratika ikiwa ni pamoja na kubadili maeneo yao ya makazi na kupelekea dhana nzima ya kusaidia kundi hili la vijana kuwa changamoto.
Jamii imekuwa na mwitikio hafifu katika kujitokeza kuunda vikundi ili viweze kusaidiwa ikiwa ni kuwezeshwa kiuchumi kupitia fedha zinazotolewa na Halmashauri ambazo ni asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.
Kaimu Afisa Maendeleo wa wilaya Bw, Abel Mosha imesisitiza kwa kusema ni kweli kama halmashauri wanapitia changamoto mbalimbali hata hivyo amesema wataendelea kutoa elimu kwa jamii ili iweze kutambua umhimu wa kuunda vikundi katika makundi haya ya Wanawake, Vijana na Walemavu kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha makundi haya yanakuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi na sikuwa tegemezi katika jamii zao.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema amesema katika kuhakikisha changamoto ya utoaji wa fedha za mikopo katika makundi ya wanawake, Vijana na Walemavu, atahakikisha anaweka utaratibu mzuri kupitia vikao vya kishera pamoja na baraza la madiwani ikiwa ni pamoja na kubuni vyazo vipya va mapto lakini pia watahakikisha wanasimamia sheria kama inavyowataka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila fedha ya mapato inayopatikana asilimia 10 ya mapato hayo inatengwa kwa ajili ya kuvipa fedha vikundi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.