Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa ahadi hiyo katika Halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza alipokuwa katika ziara maalumu ya kikazi katika Halmashauri ya Sengerema yenye lengo la kujionea utekezaji wa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na wizara yake.
Akiwa katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Sengerema Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza yimu ya menejiment kwa namna ambavyo imeweza kusimamia vizuri miradi hiyo.
Ndipo alipotoa ahadi ya zaidi ya shilingi million 500 ikiwa ni kwa ajili ya uanzishaji wa ujenzi wa wodi pamoja na theatre katika kituo cha Afya Kamanga na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Kachuo katika kata ya Nyamatongo.
Pia ujenzi wa maabara mbili ya Chemistry pamoja na Biology, ujenzi wa mabweni mawili la wavulana pamoja la wasichana pia msaada wa vitabu katika shule ya Sekondari Bugumbikiso kata ya Chifunfu.
Na mwisho ameahidi ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ukamilishaji wa Zahanati ya Isome katika kata ya Busilasoga.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watumishi na wafanyakazi wote katika Halmashauri ya Sengerema alisema, “sisi kama watendaji wakuu na wafanyakazi wa Halmashauri ya Sengerema tunakuahidi usimamizi uliotukuka na nidhamu ya hali ya juu katika fedha zote utakazo leta kwa ajili ya miradi ya maendeleo”
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.