Mbunge wa Jimbo la Sengerema Wiliamu Ngeleja ametoa mifuko 200 ya saluji yenye thamani ya ya zaidi ya shilingi miloni 3 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari Katunguru katika halmashauri ya Sengerema iliyokubwa na janga la moto.
Akikabidhi mifuko hiyo jana kwa niaba ya Mbunge huyo Diwani wa Kata ya Katunguru Mathew Lubongeja amesema amefikia maamuzi hayo ili kuwasaidia wananchi wake ambao watoto wao wamepata madhara makubwa ya kuunguliwa na vitu vyao na kukoswa mahara pa kulala, alisema
“Ngeleja anawapapole walimu na wanafunzi ambao wamepata adha hiyo na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na itahakikisha wanatoa mchango wa hali na mali ili kurejesha miundu mbinu ya bweni hilo ili watoto waweze kupata mahala salama pa kusomea na kujifunzia kama hapo mwanzo”
Mwalimu wa taaruma wa shule hiyo Bwn. Anton Bulugu amesema kumekuwepo na athari za kitaaruma kwa wanafunzi hao na kusema, wamekosa masomo kwa muda siku kadhaa sasa hivyo jamii na serikali inapaswa kuliangalia swala hilo kwa mapana ili kuwasaidia.
Nae Mkuu wa shule ya Sekondary Katunguru Baraka Msimba ameshukuru kupokea msaada huo na kusema itamsaidi kusukuma ujenzi wa bweni jipya ambao umeanza na kuwaomba wananchi wengine wajitolea kuwasaidia ili wanafunzi hao waweze kupata mahari pa kulala, ameongeza kwa kusema kuwa “hadi sasa amekwisha pokea magodoro 160 yaliyotolewa na kamati ya ulinzi la mkoa wa mwanza pamoja na kamati ya ulinzi ya wilaya ya sengerema kwa ajili ya wanafunzi walionguliwa bweni lao”
Nao wanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondary Katungurua wamesema kuwa baada ya moto huo kutokea hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyeendelea na kusoma kilichotokea wengi wetu tulizilai na kuomba msaada.
Mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo amesema tukio hilo limerudisha nyuma maendeleo ya watoto wao hivyo wanaomba Serikali kuwasaidia ili kumaliza tatizo hilo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.