Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka wananchi wa Sengerema na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kulinda na kutunza ziwa Victoria kwa kukomesha uvuvi haramu katika ziwa hilo.
Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji na usafi wa Mazingira uliogharimu fedha za kitanzania zipatazo Bil. 22.4 Wilayani Sengerema mkoani hapa.
Mh. Rais, amesema nilazima suala la uvuvi haramu likemewe kwa nguvu zote na kwa ngazi zote, “Nimeambiwa wapo baadhi ya watu kwa kushirikiana na watumishi wa umma wasio wa aminifu wanaendesha uvuvi haramu, nitoe wito kwa yeyote atakaye bainika kufanya hivyo, serikali haitakuwa na msamaha kwake” alisema Mh. Rais.
Rais Magufuli amesema, mtu anapotumia sumu ziwani anauwa hata viumbe visivyo husika na zaidi sana dawa zinazotumika kusafisha maji hazina uwezo wakuondoa kemikali, hivyo nilazima kila mwananchi aelewe kutumia sumu ya thiodani ziwani ni hatari kwa maisha yao.
Ameongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo ni kukamilisha aliyo ahidi katika kampeni zake wakati akiomba kura ambapo, kwa sasa wananchi wa Sengerema watapata maji kwa asilimia 100.
Kwa upande wake, Waziri maji Mhandisi Gerson Lwenge, amesema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 15.84 na kunufaisha wakaazi wapatao 138,000 wa mji wa Sengerema na vijiji vya jiarani vya Nyamazugo, Kijuka, Mwaliga na Nyamizeze kwa asilimia 100 hadi kufikia mwaka 2030.
Awali akitoa salaam za Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema mka huo kwa sasa umjipanga kikamilifu kwenye mageuzi ya Mapinduzi ya viwanda, huku akimakikishia Mh. Rais uwepo wa Viwanda 12 vikubwa ambavyo vipo tayari kwakufunguliwa.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema, mkoa umeamua kuweka nguvu kubwa katika zao la Pamba, ‘Mh. Rais katika Msimu wa 2016/2017 mavuno yetu ya Pamba yalifikia tani Mil.5, lakini katika msimu huu, tunatazamia kupata sio chini ya tani Mil. 20.
Naye Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Sengerema alisema, wanamshukuru sana Mh. Rais kwakuendelea kuwatumikia watanzania kwa moyo wa uaminifu lakini zaidi sana kukamilisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo inayo himiza kuwa na maji safi na salama kwa Vijijini kwa asilimia 85 na mijini asilimia 95,
“Mh. Rais yawezekana ni kweli wananchi wa Sengerema waliteseka kwa muda mrefu, lakini sisi wanasiasa yawezekana tulikuwa na shida kubwa zaidi, maana mradi huu umekuwa wa muda mrefu na mahali pengine hata tulipokuwa tukiongewa walikuwa hawatuelewi majukwaani” alisema Ngeleja.
Kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Sengerema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ni ishara kwamba Mji wa Sengerema sasa utapata maji kwa asilimia miamoja ambapo wananchi wapatao 138,000 watanufaika na mradi huo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.